IQNA

Saudia inawatimua wakimbizi Waislamu Warohingya

11:23 - January 09, 2019
1
Habari ID: 3471801
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umeanza mradi wa kuwatimua wakimbizi Waislamu wa jamii wa Rohingya ambao walikimbia mateso na mauaji ya kimbari katika nchi yao ya jadi, Myanmar.

Kwa mujibu wa taarifa, maafisa wa usalama wa Saudi Arabia wamewakamata Warohingya na kuwapelekea katika kambi ya Wakimbizi ya Shumasi mjini Jeddah ambapo wanashikiliwa kabla ya kusafirishwa kwa lazima hadi Bangladesh.

Idadi kubwa ya wakimbizi hao Warohingya waliingia Saudi Araia kwa visa za Umrah au Hija lakini wakaamua kubakia nchini humo wakihofia kuuawa au kuteswa endapo watarejea Myanmar. Halikadhalika kuna baadhi ya Warohingya ambao wamezaliwa Saudi Arabia lakini sasa wanakamatwa na kupelekwa katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh.

Nay San Lwing, mwanaharakati Mrohingya anayeishi Frankfurt Ujerumani amesema aghalabu ya Warohingya waliingia Saudi Arabia mwaka 2012 kufuatia kuibuka mapigano katika jimbo la Rakhine. Anasema Warohingya wanaotimuliwa Saudi Arabia wanalazimishwa kuenda kuishi katika kambi za wakimbizi nchini Bangladesh.

Jinai kubwa wanazofanyiwa Waislamu hao na wanajeshi na Mabudha wa nchi hiyo  wenye misimamo ya kufurutu katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa Myanmar zilishika kasi tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka 2017. Hadii sasa  jina hizo zimepelekea kuuliwa Waislamu zaidi ya elfu saba na kujeruhiwa maelfu ya wengine huku wengine zaidi ya laki nane wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani za Bangladesh na India.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya jeshi la Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Pamoja na kuwa Waislamu wa Myanmar wanakabiliwa na hali hiyo ya kusikitisha Saudi Arabia, ambayo watawale wake wanajinadi kuwa eti ni 'wahudumu wa Haram Mbili Takatifu za Kiislamu' wanawtimua Waismau Warohingya waliokimbilia hifadhi nchini humo.

3467651

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
Ni kiburi tu hakuna jingine...
captcha