IQNA

Watu 30 Wasilimu Iran katika Haram ya Bibi Masoomah SA mjini Qum

11:24 - January 27, 2019
Habari ID: 3471821
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya watu 30 kutoka nchi mbali mbali wameukumbatia Uislamu maishani baada ya kutembelea Haram Takatifu ya Bibi Masoomah SA katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran katika kipindi cha mwaka moja uliopita.

Kwa mujibu wa Kamal Suraya Ardakani Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika Ofisi ya Mfawidhi wa Haram ya Bibi Masoomah SA. Amesema waliosilimu katika haram hiyo takatifu ni kutoka nchi kama vile Korea Kusini, Japan, Brazil, Mexico, Uswisi, Ujerumani, Ufaransa, Uchina na Luxemburg.

Amesema idara yake ina mipango maalumu ya kuwasaidia waliosilumu na inadumisha mawasiliano nao. Aidha amesema tokea Machi 20, 2018 hadi sasa zaidi ya raia wa kigeni 16,000 kutoka nchi 86 wametembelea Haram Takatifu ya Bibi Masoomah SA.

Inafaa kuashiria hapa kuwa,Bibi Fatima al Masoomah SA ni binti wa Imamu wa Saba,  Imam Mussa bin Jaafar al Kadhim AS na ni kaka Imam Ridha AS.

Tarehe 23 Rabiul Awwal mwaka 201 Hijiria Bibi Fatima al Maasuma aliwasili katika mji mtukufu wa Qum. Aliishi katika mji huo kwa siku 17 na katika wakati huo alijishughulisha na ibada, dua na kujikurubishwa kwa Mola Muumba.

Eneo alilokuwa akifanyia ibada bibi huyo mtukufu hadi leo linajulikana kama 'Baitul Nur, na hadi leo linatembelewa na wapenzi wa Ahlul Bait wa Mtume Muhammad SAW.

Mwishowe tarehe 10 Rabiul Thani mwaka 201 Hijiria Bibi Fatima al Bibi Masoomah SA alifariki dunia. Watu wa Qum na wapenzi wa Ahlul Bait waliuzika mwili wa bibi huyo mtukufu katika eneo ambalo wakati huo lilikuwa nje ya mji lililojulikana kama 'Bustani ya Babol'. Baada ya kuzikwa Mussa bin Khazarj Saibani aliweka juu ya kaburi la mtukufu huyo mikeka mingi.

Hali hiyo ilibaki hivyo hadi mwaka 256 Hijiria ambapo Bibi Zeynab binti wa Imam Jawad AS alijenga kuba la kwanza juu ya kaburi la shangazi yake huyo mtukufu, na kwa utaratibu huo eneo hilo alikozikwa mtukufu huyo wa Kiislamu, likawa kivutio cha nyoyo za wapenzi na maashiqi wa Ahlul Bait AS na wafuasi wa Maimam Watoharifu. Kutokana na baraka ya eneo hilo, hadi hii leo mji wa Qum ni moja ya vituo vikubwa vya elimu ya dini tukufu ya Uislamu duniani. 

3467797

captcha