IQNA

Waziri Mkuu Mahathir Mohamad

Malaysia inasisitiza kuwa Israel ni utawala wa kihalifu

18:44 - January 29, 2019
Habari ID: 3471824
TEHRAN (IQNA)-Waziri Mkuu wa Malaysia Mahathir Mohammad amesisitiza Jumatatu kuwa nchi yake inashikilia msimamo wake wa kuwazuia raia wa utawala haramu wa Israel kuingia nchini humo huku akiitaja Israel kuwa utawala wa kihalifu.

"Tunashikilia msimamo wetu kuwa Israel ni utawala halifu ambao umekiuka sheria nyingi za kimataifa na hakuna anayelalamikia jambo hilo. Ameongeza kuwa Malaysia ina haki ya kubainisha hisia na sera zake kuhusu kadhia hiyo.  Mahathir alikuwa akijibu swali kuhusu uamuzi wa Kamati ya Kimataifa ya Paralimpiki (IPC) kuipokonya Malaysia haki ya kuandaa mashindano ya mwaka 2019 ya Paralimiki ya Kuogelea baada ya nchi yake kuwapiga marufuku waogeleaji wa Israel kushiriki.

Mashindano hayo ya Malaysia ambayo yalikuwa ni shemu ya mchujo wa Paralimpiki ya 2020 ya Tokyo, yalikuwa yamepengWa kufanyika mjini Kuching kuanzia Julai 29 hadi Agosti 4.

Malaysia ni nchi ambayo raia wake wengi ni Waislamu na haina uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.

Mapema mwezi Januari, wakuu wa Malaysia walisema hawatawaruhusu Waisraeli kushiriki katika shughuli yoyote nchini humo. Mahathir amesema hajalishwi na uamuzi wa IPC huku akiongeza kuwa nchi yake inaweza kuandaa michezo mingine. Mahathir ameshangaa ni kwa nini hakukuwa na malalamiko ya kimataifa wakati Marekani ilipowazuia raia wa nchi tano za Waislamu kuingia nchini humo.

Amesema ni jambo la kawaida kimataifa kwa nchi kuwazuia raia wa nchi fulani kwa sababu ya sera inazofuata. Malaysia imekuwa mstari wa mbele kuwatetea Wapalestina wanaopigania ukombozi wa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Wakati huo huo Balozi wa Palestina nchini Malaysia, Wali Abu Ali amesema msomamo wa Mahathir Mohammad unapaswa kuungwa mkono na nchi zote zinazotetea ukombozi wa Palestina.

3467818

captcha