IQNA

Bima ya Kiislamu inazidi kustawi duniani

22:18 - April 19, 2019
Habari ID: 3471921
TEHRAN (IQNA)- Sekta ya Bima ya Kiislamu maarufu kama Takaful inatazamiwa kustawi kote duniani mwaka huu.

Kwa mujibu wa taasisi ya kimataifa ya vigezo vya kiuchumi, Moody’s, inasema katika mwaka wa 2019, kutashuhudiwa ustawi wa Bima ya Kiislamu katika nchi za Ghuba ya Uajemi, Kusini Mashariki mwa Asia na bara Afrika.

“Tunatazamia Bima ya Takaful kustawi kwa wastani katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu ijayo. Eneo la Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ni soko kubwa Zaidi la Bima ya Kiislamu hasa kutokana na ulazima wa kuwa na bima ya gari na afya. Aidha harakati za kiuchumi zitokanazo na matukio ya michezo na kiutamaduni kama vile tamasha la 2020 Expo nchini UAE na Kombe la Dunia la Fifa 2022 nchini Qatar pia zitachangia ustawi wa Bima ya Kiislamu,” amesema Mohammad Ali Londe, mchambzui wa Moody’s.

Wataalamu wakizungumza katika Kongamano la 14 la Takaful mjini Dubai mapema mwezi huu wamesema sekta hiyo ina uwezo mkubwa wa kustawi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Ustawi wa Sekta ya Kiislamu ya Fedha mwaka 2018 ambayo ilitayarishwa na taasisi ya Thomson Reuters, sekta ya Takaful duniani ilikuwa na thamani ya dola bilioni 46 mwaka 2017. Kwa ujumla kuna mashirika karibu 324 yanayotoa huduma za Takaful kote duniani.

Kati ya mambo mengine, bima ya takaful haitegemei riba na gharar na hivyo inafungamana na mafundisho ya Kiislamu.

3468322

captcha