IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Marekani, Saudia ni waungaji mkono wa ugaidi

9:22 - April 23, 2019
Habari ID: 3471925
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuwa Marekani na Saudi Arabia ni waungaji mkono ugaidi.

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo Jumatatu jioni katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na kanali ya Televisheni ya Al Manar kutoka mjini Beirut wakati akiwahutubia Waislamu kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake).

Katika hotuba yake, Kiongozi wa Hizbullah amesema kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) ni zao la Saudi Arabia na fikra za Uwahabi. Ameongeza  kwamba makundi mengi ya kigaidi yanapata mikopo ya fedha kutoka taasisi mbalimbali za kidini nchini Saudia na kutumia fikra hizo hizo za Uwahabi kufanya mauaji na jinai dhidi ya mataifa ya Waislamu.

Sayyed Hassan Nasrallah amebainisha kwamba kwamba uliwemungu wa Kiislamu na Kiarabu unatakiwa kutambua ukweli wa siasa haribifu za Saudia na Imarati nchini Yemen, Bahrain na uingiliaji wao nchini Sudan na Libya na kadhalika nafasi za nchi hizo katika kushirikiana na Marekani na Israel kwa ajili ya "Muamala wa Karne"

Kwa mujibu wa mpango wa Marekani wa "Mumala wa Karne", mji wa Quds (Jerusalem) utakabidhiwa kwa utawala bandia wa Israel, wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki ya kurejea kwao, utawala haramu wa Israel utasimamia usalama wa sehemu kubwa ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na vivuko vya mpakani huku maeneo pekee ya Kiarabu ya Quds Mashariki yakiunganishwa na nchi ya Palestina..

Kiongozi wa Hizbullah pia ameashiria hatua ya Marekani ya kutorefusha msamaha kwa baadhi ya nchi kwa ajili ya kununua mafuta ya Iran na kusema kuwa, kwa kuzingatia kuwa dunia nzima hivi sasa inapinga siasa chafu za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hivyo inatakiwa kuchukua maamuzi chanya kuikabili Marekani.

Aidha amesema kuwa Marekani ni muungaji mkono mkubwa wa ugaidi na maelfu ya watu wanauwa na wimbi hilo huku Washington ikitoa madai kuwa eti inapambana na ugaidi  wakati inaugawia utawala wa Kizayuni wa Israel  mji  wa Quds pamoja na milima ya Golan ya Syria.

Akibainisha kwamba raia wa Palestina wanatakiwa kuwa na matumaini, amesisitiza kwamba maadamu Wapalestina hao wanayo matumaini, basi hakuna mtu ambaye atafanikiwa kuwatwisha mpango mchafu wa Marekani wa Muamala wa Karne.

Akiendelea na hotuba yake amekanusha habari ya gazeti la Al Rai la Kuwait ambalo lilinukuu kauli yake vibaya kwamba eti Lebanon na utawala haramu wa Kizayuni zitaingia katika vita kwenye msimu ujao wa joto na amesema kuwa, utawala wa Israel hauna uwezo wa kuingia vita nyingine kutokana na kukosa maandalizi ya vikosi vyake vya ardhini.

Aidha Sayyed Nasrallah amekanusha uvumi kuwpeo mapignao baina ya vikosi vya Iran na Russia katika maeneo la Dayr al-Zawr  na Aleppo Syria na kusema hizo ni propaganda za Televisheni ya Al Arabia inayomilikiwa na Saudia.

3805681

Kishikizo: iqna nasrallah
captcha