IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ina umuhimu mkubwa kuliko miaka mingine

10:53 - May 30, 2019
Habari ID: 3471977
TEHRAN (IQNA) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba kulitetea taifa la Palestina ni kadhia kibinaadamu na kidini.

Akiwahutubia maelfu ya wahadhiri kutoka vyuo vikuu vya Iran mjini Tehran siku ya Jumatano, Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema Marekani inafanya jitihada za kufanikisha mpango wa 'Muamala wa Karne' lakini kwamba Washington na washirika wake watafeli tena katika kadhia hiyo.

Kiongozi Muadhamu ameitaja Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu kuwa iliyo na umuhimu mkubwa kuliko miaka mingine na kwamba sababu ya kuongezeka umuhimu huo inatokana na ongezeko la hatua za uhaini za Marekani na vibaraka wake katika eneo kwa ajili ya kufanikisha mpango huo wa Muamala wa Karne. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Ali Khamenei ameashiria propaganda za vyombo vya habari vya kigeni kuhusiana na kadhia ya mazungumzo na kubainisha kwamba, lengo la vyombo hivyo ni kuilazimisha Iran iweze kukaa kwenye meza ya mazungumzo na Marekani. Amebaini kuwa Iran haina matatizo na mataifa mengine na kwa hivyo imekuwa ikifanya mazungumzo na nchi Ulaya. Akibainisha kwamba Iran haitafanya mazungumzo na Marekani, Kiongozi Muadhamu amesema:  "Hatutafanya mazungumzo na Marekani kuhusiana na sababu zake nimezitaja mara kadhaa. Sababu ya kwanza ya kutofnaya mazungumzo na Marekani ni kuwa hayana faida na pili ni kuwa mazungumzo hayo pia yana hasara. Marekani ikitaka kufikia malengo yake katika nchi Fulani hutumia stratijia ya mashinikizo na pembeni mwa stratijia hiyo pia hutumia mbinu ya mazungumzo. Wakati Marekani inapohisi upande wa pili umechoka kutokana na mashinikizo huibua pendekezo la mazungumzo. Kwa hivyo stratijia ya Marekani ni mashinikizo."

3815690

captcha