IQNA

Sisi hatuna ruhusa ya kuishi!

Hakuna nchi yoyote inayowataka, lakini wanapaswa kulindwa. Kwa mujibu wa kauli rasmi ya jamii yakimataifa, wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya wanapaswa kurejea katika nchi yao, Myanmar, kwa hiari yao, kwa usalama na kwa heshima.

Pamoja na hayo, maafisa wa Umoja wa Mataifa wanadai kuwa, yamkini kwa muda wa miaka mingi ijayo, wakimbizi Warohingya hawataweza kurejea nchini Myanmar. Kambi ya wakimbizi Warohingya iliyoko kusini mashariki mwa Bangladesh, ina karibu wakimbizi milioni moja ambayo aghalabu ni Waislamu. Kambi hiyo hivi sasa ni kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.  Aghalabu ya watu wa kabila la Rohingya ni Waislamu na kuanzia Agosti mwaka 2017 walianza kukabiliana na mauaji ya kimbari ambayo yamekuwa yakitekelezwa na Jeshi la Myanmar.