IQNA

Kuhifadhi Qur'ani ni kigezo cha kuingia vyuo vikuu Indonesia

10:40 - July 04, 2019
Habari ID: 3472032
TEHRAN (IQNA) - Vyuo vikuu vya umma nchini Indonesia vimetangaza kuwa vijana waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu wanaweza kuingia katika vyuo vikuu pasina kufanya mtihani wa kawaida unaohitajika kuingia chuo kikuu.

Idadi kubwa ya vijana nchini Indonesia wameweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa ajili ya kujikurubisha zaidi kwa Allah SWT. Wengi huanza kuhifadhi Qur'ani wakiwa utotoni na wakati wanaopfika umri wa kuingia chuo kikuu huwa tayari wamehifadhi juzuu zote 30 za Qur'ani Tukufu.
Katika mpango huo, wanafunzi walioweza kuhifadhi Qur'ani sasa wataweza kusoma taaluma mbali mbali za sayansi ya kijamii na sanaa bila kufanya mtihani wa kawaida wa kuingia chuo kikuu.
Kwa mujibu wa mpango huo, takribani asilimia 11 ya nagasi katika kila chuo kikuu zitatengwa kwa waliohifadhi Qur'ani. Katika miaka ya hivi karibuni, idadi kubwa ya vyuo vikuu nchini Indonesia vimekuwa vikiwapa kipaumbele wanafunzi waliohifadhi Qur'ani Tukufu.

3468876

captcha