IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Iran imeanza kupunguza ahadi zaka JCPOA na itaendelea kufanya hivyo

0:32 - July 18, 2019
Habari ID: 3472047
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekosoa vikali misimamo ya nchi za Ulaya na kushindwa kwao kutekeleza ahadi zao ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kwa kusema: "Sisi ndio kwanza tumeanza kupunguza hadi zetu ndani ya mapatano hayo na bila ya shaka tutaendelea tu kupunguza utekelezaji wa ahadi zetu ndani ya JCPOA."

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema hayo Jumatano asubuhi mjini Tehran wakati alipoonana na maimamu wa Sala za Ijumaa wa kona zote za Iran na kusisitiza kuwa, mafanikio ya taifa la Iran na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu yanazidi kuwa makubwa licha ya Wamagharibi kuchukizwa sana na mafanikio hayo.

Ameongeza kuwa, tabia ya Wamagharibi ya kujiona bora inawafanya wasitake kuukubali ukweli na uhalisi wa mambo. Tab'an kiburi chao hicho kimewanufaisha mbele ya mataifa na nchi dhaifu, lakini mbele ya mataifa ambayo hayaogopi na ambayo yamesimama kidete kulinda haki zao, Wamagharibi wameshindwa kabisa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia matamshi ya wazi kabisa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kuhusu ahadi 11 za nchi za Ulaya ndani ya mapatano ya JCPOA na ambazo hakuna hata moja iliyotekelezwa na nchi hizo. Amesema: Sisi tumetekeleza hata zaidi ya ahadi zetru ndani ya mapatano hayo lakini hivi sasa baada ya kuona nchi za Ulaya hazitekelezi ahadi zao tumeamua kupunguza utekelezaji wa baadhi ya ahadi zetu, nchi za Ulaya zimekuja juu na zinahoji kijeuri kwamba kwa nini hatutekelezi ahadi zetu zote.

Katika sehemu nyingine ya miongozo yake hiyo muhimu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameilamumu vikali Uingereza kwa kuiteka nyara meli ya mafuta ya Iran tena kinyume cha sheria na kusema kuwa, hawa watu ambao usaliti wao unajulikana na kila mtu duniani, leo hii wamefanya uharamia wa kuiteka nyara meli yetu, na wanafanya njama za kuhalalisha uharamia wao huo. Lakini watu waumini ndani ya Jamhuri ya Kiislamu hawatoliacha jambo hilo lipite vivi hivi bila ya kutoa majibu; na bila ya shaka watotoa jibu linalopasa katika wakati na mahala panapofaa.

Vile vile amesema kuwa, mafanikio makubwa na ya kujivunia ya kiulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni matunda ya kuacha kabisa kuwategemea maajinabi katika kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu na kusisitiza kuwa, harakati iliyopo hivi sasa pia itazaa matunda mazuri sana kwa baraka za kujitegemea katika nyuga tofauti zikiwemo za kiuchumi.

3468977

captcha