IQNA

Msikiti wahujumiwa huko Brisbane, Australia

12:16 - September 11, 2019
Habari ID: 3472125
TEHRAN (IQNA) - Watu wanaoaminika kuwa wahalifu wazungu wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali ya kibaguzi wameuhujumu msikiti katika mji wa Brisbane, Australia.

Polisi katika Jimbo la Queensland wamethibitisha kutokea tukio hilo katika Msikiti wa Holland Park katika mji huo wa Brisbane.
Waliouhujumu msikiti huo Jumatano walichora Swastika ambayo ni nembo ya kibaguzi Wanazi katika ukuta wa msikiti. Aidha waliandika maandishi ya kutukuza jina la gaidi Tarrant aliyeua Waislamu 52 katika hujuma dhidi ya misikiti miwili katika mji wa Christchurch New Zealand mwezi Machi mwaka huu. Halikadhlika kulikuwa na maandishi ya 'Remove Kebab' ambayo yaliashiria nyama aina ya Kebab ambayo hutumiwa na aghalabu ya Waislamu wahajiri nchini Australia.
Mbunge wa chama cha Leba na mwakilishi wa eneo la Griffith, Terri Butler amelaani vikali uhalifu huo na kuutaja kuwa wenye kuchukiza.
Gaidi mwenye umri wa miaka 28 kwa jina Brenton Tarrant raia wa Australia ambaye alihusika katika mauaji ya umati ya Waislamu nchini New Zealand wakati wa Sala ya Ijumaa amekuwa akijitangaza kuwa ni mfuasi wa sera za Rais Donald Trump wa Marekani na sasa ameshikiliwa korkoroni huku kesi yake ikiendelea.

3469375

captcha