IQNA

Quran iliyoandikwa na Imam Ridha AS kuhifadhiwa katika jumba la makumbusho la haram ya Mash-had.

12:06 - November 08, 2008
Habari ID: 1705657
Ofisi ya haram ya Imam Ridha imetangaza kwamba Qurani hiyo inayonasibishwa kwa mjukuu huyo wa Mtume Muhammad SAW imeandikwa kwa herufi za Kikufi juu ya ngozi ya swala na ina kurasa 27.
Mtaalamu wa jumba la makumbusho la Qurani la haram ya Imam Ridhaa AS bwana Rahmati ameliambia Shirika la Habari za Qurani la Kimataifa (IQNA) kwamba Qurani iliyoandikwa kwa mkono wa Imam Ridha AS inajumuisha sehemu ya sura za Nur, Qasas, Ankabuut, Rum, Luqman, Sajda, Ahzab, Fussilat, Jathiyah, Muuminun, Ahqaf, Waqiah na Hadid.
Rahmati amesema, katika ukurasa wa pili wa Qurani hiyo ambao ni mwisho wa suratul Nur, kuna maandishi: “Imeandikwa na Ali bin Mussa al Ridha” na kuna mihuri kadhaa ya wahusika wa wakati huo.
Amesema kuwa miongoni mwa sifa makhsusi za mandishi hayo ya Qurani ya Imam Ridha AS ni kuzingatia misingi ya nahau na sarafu za lugha ya Kiarabu, shada, mada na alama nyinginzo za tajwidi na usomaji wa Qurani Tukufu. 316850
captcha