IQNA

Zaidi ya anuani 800 za vitabu kidini na Qurani vya watoto katika Maonyesho ya Qurani

18:40 - August 23, 2010
Habari ID: 1979669
Jumuiya ya wachapishaji vitabu vya watoto na vijana Iran imewasilisha zaidi ya anuani 800 za vitabu vya kidini na Qurani katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qurani ya Tehran.
Amir Eliyasi Mehr mkuu wa kibanda cha Jumuiya ya wachapishaji vitabu vya watoto na vijana Iran amemuambia mwandishi wa IQNA kuwa ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki katika maonyesho ya Qurani, vitabu vya jumuiya hiyo vimepata umaarufu miongoni mwa wananchi.
Amesema jumuiya hiyo ina wanachama 58 ambao wanajisughulisha na uchapishaji na 30 kati yao wanachapishwa vitabu vya kidini na Qurani Tukufu.
Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qurani ya Tehran yalianza tarehe 27 mwezi wa Shaaban na yanatazamiwa kumalizika tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
639684
captcha