IQNA

Dini ya Kiislamu imepata nguvu duniani

18:46 - November 17, 2010
Habari ID: 2033518
Khatibu wa Sala ya Idul Adha iliyosaliwa Jumatano mjini Tehran amesema dini ya Kiislamu imepata nguvu kubwa duniani na kuvunja imani ya maadui.
Ayatullah Ahmad Khatami ameongeza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yameonyesha kuwa madola yenye nguvu a yaliyojikita kwenye makasri ya vioo yanaweza kushindwa na muqawamah wa mataifa. Khatibu wa Sala ya Idul Adha amebainisha kuwa kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, nadharia mbili za Ukomunisti na Uliberali wa Kidemokrasia ndizo zilizokuwa zikitawala duniani, na kuongeza kuwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nadharia ya Kikomunisti ilisambaratika na kwamba ile ya Uliberali wa Kidemokrasia nayo pia imo katika hali ya kuporomoka. Ayatullah Khatami amefafanua kuwa kuna wakati Marekani ilikuwa ikidhani kuwa ndio yenye kauli ya mwisho katika Mashariki ya Kati, lakini hivi sasa imenasa kwenye kinamasi cha Afghanistan na Iraq na wananchi wa mataifa hayo wanaichukia mno nchi hiyo. Aidha amesisitiza kwamba vita vya siku 33 vya Lebanon na vya siku 22 huko Gaza vimefuta ile dhana kwamba utawala wa Kizayuni haushindiki.
697266

captcha