IQNA

‘Qurani , Kitabu cha Mwamko wa Kiislamu’ ndio kauli mbiu ya maonyesho ya Qurani Iran

15:37 - April 06, 2011
Habari ID: 2101730
Kauli mbiu ya maonyesho ya 19 ya Qurani Tukufu ya Tehran imetangazwa kuwa ni ‘Qurani, Kitabu cha Mwamko wa Kiislamu’.
Katika kikao kilichofanyika Aprili nne wahusika wa maonyesho hao akiwemo Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Seyyed Mohammad Husseini wamechukua uamuzi wa kauli mbiu hiyo kwa kuzingatia matukio ya mwamko wa Kiislamu duniani.
Husseini amesema maonyesho hayo ni tukio muhimu la Qurani, kidini na kiutamaduni . Ameongeza kuwa maonyesho ya kimataifa ya Qurani Tehran yanafanyika kutokana na juhudi za pamoja za wahusika kote Iran.
‘Iran ni nchi ya Kiislamu na kwa hivyo masuala ya Qurani yanapaswa kupewa umuhimu mkubwa’ amesema.
‘Pale mafundisho ya Qurani yatakapodhihiri katika maisha ya wote basi jamii itashuhudia ustawi mkubwa’ amesisitiza.
Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu amesema kuwa maonyesho ya mwaka huu yatazingaita suala la kukabiliana na wale wanaoeneza chuki dhidi ya Qurani Tukufu aidha suala la Jihadi ya Kiuchumi litazingatiwa pia katika maonyesho hayo.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qurani hufanyika kila mwaka mjini Tehran katika Ukumbi Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini MA katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
769059
captcha