IQNA

Kikao cha kukosoa filamu ya Hassan na Hussein kufanyika IQNA

15:42 - October 10, 2011
Habari ID: 2202478
Kikao cha kuchunguza na kukosoa filamu na al Hassan na al Hussain inayopigavita madhehebu ya Shia kitafanyika kesho mjini Tehran kwa ushirikiano wa Shirika la Habari za Qurani la Kimataifa IQNA na kanali ya televisheni ya al Alam.
Kikao hicho kitakuwa cha kwanza katika mfululizo wa vikao kadhaa vya kuchunguza na kukosoa filamu hiyo.
Ayatullah Muhammad Hadi al Yusufi al Gharawi mhadhiri wa vyuo vikuu na mtunzi wa kitabu kikubwa cha historia ya Kiislamu na Sayyid Khalil Bastan mjumbe wa Baraza Kuu la Chuo Kikuu cha Allamah Tabatabai mjini Tehran watachambua na kuchunguza filamu hiyo.
kikao hicho kitarushwa hewani baadaye na kanali na satalaiti ya televisheni ya al Alam na vyombo vingine vya habari.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa filamu ya al Hassan na al Hussan inapiga vita itikadi za madhehebu ya Shia na kupotosha historia ya Kiislamu. Filamu hiyo ambayo imetengenezwa kwa himaya na fedha za Mawahabi mbali na kusafisha sura ya Muawiyah bin Abi Sufiyan, inataka kuonesha kwamba Ahlul Bait wa Mtume SAW hawana tatizo lolote na mtu huyo na kwamba mwanaye Yazid bin Muawiyah aliyemuua shahidi mjukuu wa Mtume SAW Imam Hussein AS, hana hatia yoyote. 876809
captcha