IQNA

Magaidi wa ISIS wahujumu Msikiti nchini Yemen

16:31 - October 07, 2015
Habari ID: 3382986
Magaidi wa kundi la ISIS au Daesh wameshambulia kwa bomu Masjid Nur jana Jumanne katika mtaa wal al-Nahda katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a ambapo watu saba wamepoteza maisha.

Halikadhalika hivi karibuni wakati wa Sala ya Idul Adha, magaidi waliushambulia kwa bomu Msikiti wa al Balili mjini Sana’a.
Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limedai kuhusika na hujuma hizo. Misikiti imekuwa ikilengwa na magaidi wa Daesh na pia ndege za kivita za Saudia zinazoendeleza hujuma dhidi ya Yemen.
Saudi Arabia ilianza kuishambulia Yemen tarehe 26 Machi mwaka huu kwa lengo la kuiondoa madarakani harakati ya Ansarullah. Mashambulizi hayo ya Saudia yameua Wayemen wasio na hatia zaidi ya 6,200 wengi wao wakiwa ni raia hasa wanawake, watoto wadogo na wazee. Saudia pia imedondosha mabomu katika misikiti, shule, viwanda na mahospitali katika maeneo mbalimbali ya Yemen.../mh

3379350

captcha