IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya walemavu wa macho kufanyika Iran

15:02 - April 13, 2016
Habari ID: 3470246
Duru ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani maalumu kwa walemavu wa macho yatafanyika Tehran sambamba na mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya kila mwaka.

Mashindano hayo yameandaliwa na Shirika la Ustawi wa Jamii la Iran na yatafanyika kuanzia Mei 12-17.

Mwakilishi wa Iran katika mashindano hayo ni Abdol Ghafouri Joharchi ambaye alishika nafasi ya pili katika mashindano ya kitaifa ya Iran huku Saeed Ali- Akbari ambaye alishika nafasi ya kwanza akipangwa kuiwakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Uturuki.

Zaidi ya nchi 30 tayari zimeshatangaza kutuma wawakilishi wao katika mashindano hayo ya wenye ulemavu wa macho.

Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya Qur’ani ya wenye ulemavu mwaka huu yatakuwa na kategoria ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu lakini kategoria nyingine zitaongezwa katika mashindano ya mustakabali.

Kwa mujibu wa wanaoandaa duru ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani maalumu kwa walemavu wa macho, mashindano ya mwaka huu yatakuwa ni ya wanaume pekee na wale wanaotaka kushiriki wanapaswa kuwa wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu. Aidha wanatakuwa kutuma faili yao ya qiraa na pia cheti cha kuonyesha kuwa wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Kila mshiriki ataruhusiwa kuwa na mtu mmoja wa kumsaidia na waandalizi watagharamia usafiri wa wote wawili, hoteli na pamoja na malazi.

Kwa maelezo Zaidi unaweza kuwasiliana na nambari zifuatazo.

+98 9193144311

+98 9127508297

Email: h.hamidi92@yahoo.com

3459522

Kishikizo: iran mashindano
captcha