IQNA

Nchi 25 kushirki mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya walemavu wa macho Iran

18:46 - April 25, 2016
Habari ID: 3470272
Nchi 25 zimethibitisha kushiriki katika awamu ya kwanza ya ashindano ya Kimataifa ya Qur'ani maalumu kwa walemavu wa macho nchini Iran.
Hujjatul Islam Seyyed Mustafa Husseini, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Awqaf na Masuala ya Kiislamu Iran amemwmabia mwandishi wa IQNA kuwa, Iraq, Indonesia, Uturuki , Afghanistan na Malaysia ni kati ya nchi zilizothibitisha kutuma washiriki katika mashindano hayo.
Amesema Iran itawakilishwa katika mashindano hayo na Abdul Ghafur Joharchi kutoka eneo la Taybad, kaskazini mashariki mwa mkoa wa Khorassan Razavi.
Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya Qur’ani ya wenye ulemavu mwaka huu yatakuwa na kategoria ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu lakini kategoria nyingine zitaongezwa katika mashindano ya mustakabali.
Mashindano hayo ya Qur'ani maalumu kwa walemavu wa macho yameandaliwa na Shirika la Ustawi wa Jamii la Iran na yatafanyika pembizoni mwa Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani kuanzaia tarehe 11-17 Mei katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran.
Kwa mujibu wa wanaoandaa duru ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani maalumu kwa walemavu wa macho, mashindano ya mwaka huu yatakuwa ni ya wanaume pekee na wale wanaotaka kushiriki wanapaswa kuwa wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

3490324
Kishikizo: iqna
captcha