IQNA

Nchi 20 zashiriki maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tehran

22:30 - June 18, 2016
Habari ID: 3470396
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran mwaka huu yameshuhudia ongezeko la washiriki kutoka nchi mbali mbali duniani.
Mkuu wa Kamati ya Kimataifa katika Gholam Reza Noui amesema kuwa Maoneysho ya 24 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran yana washiriki kutoka nchi 20 za kigeni ikiwa ni pamoja na nchi kadhaa za Ulaya, Afrika Kaskazini na nchi za Kiislamu zinazopakana na Iran.
Ameongeza kuwa, kuna wataalamu wa Qur'ani kutoka nchini 15 wanaoshiriki katika maonyesho ya mwaka huu.
Kati ya nchi za kigeni zinazoshiriki maonyesho ya mwaka huu ni Algeria, Uturuki, Iraq na Italia.
Maonyesho ya mwaka huu ambayo yalianza tarehe Mosi mwezi Mtukfuu wa Ramadhani na kufunguliwa rasmi tarehe 13 Juni yanatazamiwa kumalizika 30 Juni. Maonyesho hayo yana vibanda 300 huku kitengo cha vitabu kikiwa kikubwa zaidi.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran ni makubwa zaidi ya aina yake duniani.

Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran ambapo huwa na vitengo kadhaa vya maudhui mbali mbali za Qur'ani.
captcha