IQNA

Tamsha la Kimataifa la Imam Ridha AS kushirikisha nchi 77

9:38 - August 03, 2016
Habari ID: 3470491
Tamasha la Kimataifa la mjukuu wa Mtume SAW, Imam Ridha AS, litafanyika nchini Iran na kushirikisha nchi 77 mwaka huu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, ICRO, Dkt. Abuzar Ebrahimi Torkaman amesema tamasha hilo ambalo lilianza miaka 14 iliyopita litafanyika kwa mara ya saba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran Jumanne, amesema tamasha hilo ni la Sanaa na utamaduni na hujumuisha kazi kumhusu Imamu wa Nane wa Madhehebu ya Shia, Imam Ridha AS, limewavutia wasanii na wasomi waandishi wa vitabu ambao huonyesha mahaba yao kwa Imam Ridha AS.

Amesema ICRO inandaa tamasha hilo kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW, Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, Taasisi ya Kimataifa ya Imam Ridha AS, Taasisi ya Kusimamia Haram ya Imam Ridha AS na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS.

Kati ya nchi zitakazoshiriki ni pamoja na Uganda, Tanzania, Madagascar, Mali, Myanmar, India, Bangladesh, China, Myanmar, Tajikistan na Georgia.

Halikadhalika kutakuwa na matamsha madogo katika maeneo 2400 kote duniani.

Tamasha la Kimataifa la Imam Ridha AS litaanza Agosti 11 katika mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

3519651

captcha