Bismillahir Rahmanir Rahim.
Na
hamdu na shukrani zote zinamstahikia Allah, Mola Mlezi wa viumbe wote.
Na rehema na amani ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad na Aal zake
watoharifu na masahaba wake wateule na wote waliowafuata hao kwa wema
hadi Siku ya Kiyama.
Ndugu zangu makaka na madada Waislamu kote ulimwenguni!
Msimu
wa Hija kwa ajili ya Waislamu ni msimu wa kujifakharisha nao, ni msimu
wa kujivunia mbele ya macho ya walimwengu. Msimu wa Hija ni wa
kuzinawirisha nyoyo na kuingiza humo khushuu na unyenyekevu mbele ya
Muumba. Hija ni faradhi tukufu ya kidunia, Kiungu na kiwatu. Hija ni
faradhi itokanayo na amri ya Mwenyezi Mungu aliposema:
فَاذْكُرُواْ اللَّهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا
Basi mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu au mtajeni zaidi. Na amri inayosema:
وَاذْكُرُواْ اللَّهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ
Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku chache zinazohisabika.
Vile vile Hija inatokana na maneno ya Mwenyezi Mungu aliposema:
الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاء الْعَاكِفُ فِيهِ وَالْبَادِ
(Msikiti Mtakatifu wa Makkah) Ambao tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni.
Yote hayo yanabainisha kwa uwazi vipengee visivyo na kifani na hali tofauti za Hija.
Katika
faradhi hii ya kidini isiyo na mfano, suala la usalama wa wakati na
sehemu ni mithili ya ishara iliyo wazi na nyota inayong'ara ambayo
inazipa utulivu nyoyo za watu na kumtoa hujaji kutoka katika mzingiro wa
mambo yanayovunja usalama yanayosababishwa na madhalimu mabeberu ambayo
daima yamekuwa yakitishia usalama wa wanadamu, na hatimae kumpa hujaji
furaha ya usalama katika kipindi fulani maalumu.
Hija ya Kiibrahimu
ambayo ni zawadi waliyopewa Waislamu na (dini tukufu ya) Uislamu, ni
dhihirisho la heshima, umaanawi, umoja na adhama; inawadhihirishia kwa
uwazi kabisa maadui na wale wanaowatakia mabaya Waislamu, utukufu wa
umma wa Kiislamu na kutegemea kwao nguvu isiyo na kikomo ya Mwenyezi
Mungu, na vile vile kuchora picha ya namna wanavyoweza kuwa mbali na
karo za ufisadi, udhalilishaji na udunishaji; mambo ambayo mabeberu na
waistikbari wa kimataifa wamezitishwa jamii za wanadamu duniani. Hija ya
Kiislamu na kitauhidi, ni dhihirisho la kweli la aya ya Qur'ani Tukufu
inayosema:
أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُمْ
...wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao.
Hija ni mahala pa kujibari na kujiweka mbali na washirikina na ni mahala pa kutia nguvu umoja na mshikamano wa waumini.
Wale
watu ambao wameifanya Hija kuwa ni safari ya kitalii na matembezi ambao
wanaficha chuki zao kwa taifa la waumini na wanamapinduzi la Iran ndani
ya madai ya kukataa kuingiza siasa ndani ya Hija, ni mashetani dhalili
na duni ambao wanatetemeka wanapoona tamaa za shetani mkubwa Marekani
zinaingia hatarini. Watawala wa Kisaudi ambao mwaka huu wamewazuilia
njia ya Mwenyezi Mungu na Masjidul Haram na kuwafungia njia mahujaji
wenye ghera na waumini wa Kiirani wasiweze kufanya ibada katika nyumba
ya Mahbubu wao, ni watu waovu waliopotea ambao wanaona kuwa hawawezi
kubakia kidhulma katika madaraka ila kwa kuwalinda waistikbari na
mabeberu wa dunia na kuwa waitifaki wa Uzayuni na Marekani ambao muda
wote wanafanya juhudi za kuwakidhia waistikbari hao matakwa yao;
hawasiti hata kidogo kufanya usaliti wa aina yoyote ile kwenye jambo
hilo.
Hivi sasa karibu mwaka mzima umepita tangu lilipotokea tukio la
kutisha la Mina. Ndani ya tukio hilo, maelfu kadhaa ya mahujaji
waliokuwa katika nguo za Ihram, chini ya jua na midomo yenye kitu
waliuawa kidhulma ndani ya siku ya Idi. Siku chache kabla ya tukio hilo,
majimui ya mahujaji waliokuwa katika ibada na katika hali ya kutufu na
kusali waliuawa ndani ya Masjidul Haram. Watawala wa Kisaudi ndio wa
kulaumiwa katika matukio yote hayo mawili; na hicho ni kitu ambacho
kinakubaliwa kwa kauli moja na watu wote waliokuwepo, wachunguzi na kila
aliyeyafanyia utafiti kiutaalamu matukio hayo; bali wako baadhi ya
wataalamu wanazungumzia uwezekano wa kwamba jambo hilo lilifanywa kwa
makusudi. Kupuuza na kufanya uzembe katika kuwaokoa mahujaji ambao
walikuwa hawajakata roho ambayo nyoyo zao ambao roho zao zenye shauku na
nyoyo zao zenye hamu katika Siku ya Idi ya Kuchinja ziliambatana na
ndimi zao zilizokuwa zikimtaja Allah kwa dhikri na kusoma aya za maneno
ya Mwenyezi Mungu. Wasaudi watenda jinai na wenye nyoyo ngumu
waliwachukua majeruhi hao na kuwafungia kwenye makontena pamoja na
mahujaji waliofariki dunia; na badala ya kuwatibu na kuwasaidia au hata
kuwafikishia maji katika midomo yao iliyokuwa na kiu (kali), waliwaua
shahidi (mahujaji hao ambao walikuwa bado hawajakata roho). Maelfu
kadhaa ya familia kutoka nchi mbalimbali zilipoteza wapendwa wao na
mataifa yao yakapatwa na msiba. Kulikuwa na karibu mashahidi laki tano
katika mashahidi hao kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Nyoyo za
familia zao bado zimejeruhika na zina msiba, huku taifa nalo likiwa bado
limo katika majonzi na limekasirika.
Badala ya watawala wa Kisaudi
kuomba radhi, kujuta na kuwafuatilia kisheria wahusika wa moja kwa moja
wa tukio hilo la kutisha; ndio kwanza wanakataa - kijeuri kabisa na bila
ya kuona haya - hata kuunda tume ya kimataifa ya Kiislamu ya kutafuta
ukweli kuhusu tukio hilo; na badala ya watawala hao kukaa kwenye kizimba
ya mtuhumiwa, wamekaa nafasi ya mdai na kuzidi kudhihirisha na kuonesha
uadui wao wa muda mrefu - kikhabithi na kipuuzi - kwa Jamhuri ya
Kiislamu na kwa kila bendera ya Kiislamu inayopeperushwa kwa ajili ya
kukabiliana na ukafiri na Uistikbari.
Honi zao za kipropaganda;
kuanzia wanasiasa wao ambao mienendo yao kuhusu Wazayuni na Marekani ni
aibu kwa ulimwengu wa Kiislamu hadi mamufti wao wasio wacha Mungu na
walaharamu ambao wanatoa fatwa zinazokwenda kinyume kabisa na Kitabu na
Sunna, na hadi kundi la vyombo vyao vya habari ambavyo hata maadili yao
ya kiutaalamu hayawazuii kutunga na kusema uongo, wanafanya njama za
kipuuzi kuituhuma Jamhuri ya Kiislamu kuwa eti ndiyo iliyosababisha
mahujaji wa Iran wasiende kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu. Watawala
waenezaji fitna wa Kisaudi ambao wameanzisha ya kuyatia nguvu makundi ya
kitakfiri na ya kishari, yameutumbukiza ulimwengu wa Kiislamu katika
vita vya ndani na kuuliwa na kujeruhiwa watu wasio na hatia na ambao
mikono yao imejaa damu za watu hao katika nchi za Yemen, Iraq, Sham,
Libya na katika nchi nyinginezo duniani; wacheza siasa ambao hawamuogopi
Mwenyezi Mungu ambao wameunyooshea mkono wa urafiki utawala vamizi wa
Kizayuni, na kuwasababishia masaibu na mateso makubwa Wapalestina na
kupanua wigo wa dhulma na usaliti wao hadi katika miji na vijiji vya
Bahrain; watawala wasio na dini wala maadili ambao hata nyoyo zao
haziwasuti na ambao wamesababisha maafa makubwa ya Mina ambao wamevunja
utukufu wa Haram yenye usalama ya Mwenyezi Mungu kwa jina la watumishi
wa Haram mbili tukufu na ambao wamewatoa muhanga wageni wa Mwenyezi
Mungu Mwingi wa rehema katika siku ya Idi huko Mina na kabla ya hapo
ndani ya Masjidul Haram; hivi sasa wanapiga domo la kukataa kuingizwa
siasa katika Hija na wanawatuhumu wengine kufanya madhambi makubwa
ambayo ni wao wenyewe walioyafanya au kusabibisha kutokea kwake.
Watawala hao ni ‘misdaki' na dhihirisho kamili la maneno yaliyo wazi ya
Qur'ani Tukufu yanayosema:
وَ اِذا
تَوَلّىٰ سَعىٰ فِی الاَرضِ لِیُفسِدَ فیها وَ یُهلِکَ الحَرثَ وَ النَّسلَ
وَ اللّهُ لا یُحِبُّ الفَساد * وَ اِذا قیلَ لَهُ اتَّقِ اللّهَ
اَخَذَتهُ العِزَّةُ بِالاِثمِ فَحَسبُهُ جَهَنَّمُ وَ لَبِئسَ المِهاد
Na anapotawala hufanya juhudi katika ardhi kufanya ufisadi humo, na huangamiza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi. Na akiambiwa: Mche Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kutenda madhambi. Basi huyo inamtosha Jahannam, nayo ni makao mabaya mno.
Mwaka
huu pia kwa mujibu wa ripoti mbali mbali zilizotolewa, mbali na
kuwazuia mahujaji wa Kiirani na wa mataifa mengine, mahujaji wa nchi
nyinginezo nao wanadhibitiwa kwa njia isiyo ya kawaida kwa msaada wa
mashirika ya kijasusi ya Marekani na utawala wa Kizayuni, na nyumba ya
Mwenyezi Mungu iliyo salama, imekuwa haina salama kwa watu wote.
Ulimwengu mzima wa Kiislamu, iwe ni tawala au wananchi Waislamu wa nchi
hizo, wanapaswa kujua vizuri uhakika wa kutisha na ukosefu wa imani wa
watawala wa Kisaudi na namna watawala hao walivyotekwa na mambo ya
kimaada; na haupaswi kuwaacha vivi hivi watawala hao kutokana na jinai
walizousababishia ulimwengu wa Kiislamu. Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa
kufikiria kwa kina suala la kusimamia haram mbili tukufu na suala zima
la Hija kutokana na vitendo vya kidhulma vilivyofanywa na watawala hao
dhidi ya wageni wa Mwingi wa rehema. Kufanya uzembe katika kutekeleza
jukumu hilo, kutauutumbukiza mustakbali wa umma wa Kiislamu katika
matatizo makubwa zaidi.
Ndugu zangu Waislamu, wake kwa waume! Mwaka
huu nafasi ya mahujaji wenye shauku na ikhlasi wa Kiirani iko wazi
katika ibada ya Hija, lakini mahujaji hao wako pamoja na mahujaji
wengine kutoka kona zote za dunia kwa nyoyo zao, na wanawaombea dua ili
mti uliolaaniwa wa mataghuti kuwasababishia madhara yoyote yale.
Wakumbukeni ndugu zenu wa Iran katika dua na katika ibada na kunong'ona
kwenu na Mwenyezi Mungu na ombeni dua Mwenyezi Mungu aziondolee matatizo
jamii za Waislamu na aukate mkono wa waistikbari na Wazayuni na
vibaraka wao katika umma wa Kiislamu.
Ninapenda kuitumia fursa hii
kuwakumbuka na kuwaenzi mashahidi wa Mina na wa Masjidul Haram na
mashahidi wa Makka wa mwaka 1366 (Hijria Shamsia sawa na Julai 31, 1987)
[*13] na ninamuomba Mwenyezi Mungu ‘Azza Wajalla, awape maghufira,
awarehemu na awanyanyue daraja za juu za utukufu. Ninamuombea rehema
Imam wa zama (Imam Mahdi AF - roho yangu iwe fidia kwake) nikiomba dua
yenye kutakabaliwa ya mtukufu huyo iwe sababu ya kupata utukufu umma wa
Kiislamu na kuwaokoka Waislamu mbele ya fitna na shari ya maadui.
Na Taufiki ni ya Mwenyezi Mungu, Naye Ndiye Mbora wa kutegemewa.
Sayyid Ali Khamanei
Mwishoni mwa Mfunguo Pili Dhul Qaad 1437 (Hijria)
12/06/1395 (Hijria Shamsia)
(Septemba 5, 2016).
[*13]:
Maafa ya Ijumaa ya umwagaji damu ya mjini Makkah ni mfano mwingine wa
uadui wa Marekani ambayo yalitokea Mwezi Sita Mfunguo Tatu Dhil Hijja
1407 katika msimu wa Hija na baada ya kumalizika ibada ya kujibari na
kujiweka mbali na washirikina. Watawala wa ukoo wa Aal Saud waliivunjia
heshima ya amani iliyotangazwa na Mwenyezi Mungu kwa watu wanaoingia
eneo hilo na kuwaua shahidi kwa umati karibu mahujaji 400 wa Kiirani na
wasio wa Iran - wengi wao wakiwa ni wanawake - na kuwajeruhi wengine
wengi zaidi ya hao kwa mara kadhaa.