IQNA

Nakala 80,000 za Qur'ani zasambazwa Tanzania

20:23 - October 31, 2016
Habari ID: 3470645
IQNA-Shirika moja la misaada la Qatar limesambaza nakala 80,000 za Qur'ani miongoni mwa Waislamu nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Qur'ani la Kimataifa, IQNA, Shirika la Misaada la Sheikh Thani Ibn Abdullah, RAF, limesambaza nakala hizo za Qur'ani katika mradi ujulikanao kama Tibyan.

Taarifa zinasema taasisi, vituo na mashirika kadhaa ya Kiislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki yamepokea nakala hizo za Qur'ani katika hafla iliyofanyika hivi karibuni mjini Dar es Salaam.

Maafisa wa RAF wanasema lengo lao ni kueneza mafundisho ya Qur'ani na kulea kizazi cha vijana Waislamu waliohifadhi Qur'ani Tukufu.

Shirika hilo limesema hadi sasa limesambaza nakala milioni 1.2 za Qur'ani zenye tarjama kwa lugha sita za Kiafrika, Kiasia na Ulaya.

Kati ya nchi ambazo hadi sasa zimepokea nakala za Qur'ani kutoka RAF ni pamoja na Uganda, Gambia, Mauritania, Nigeria, Sierra Leone, Ufilipino, Niger, Mali na Kenya.

3542078

captcha