IQNA

Wabahrain waendeleza maandamano ya kumuunga mkono Sheikh Issa Qassima

22:16 - November 05, 2016
Habari ID: 3470654
IQNA-Wabahrain wanaendelea kuandamana mbele ya nyumba ya mwanazuoni mashuhuri wa nchi hiyo Ayatullah Sheikh Isa Qassim kwa lengo la kumuunga mkono mwanazuoni huyo anayedhulumiwa.

Ijumaa ilikuwa siku ya 138 ambapo watu wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano kila siku mbele ya nyumba ya Sheikh Qassim katika eneo la Al Diraz mjini Manama.

Mnamo Juni 2016, utawala wa kiimla wa Aal Khalifa ulimvua uraia Sheikh Qassim hatua ambayo inaendela kulaaniwa vikali na Wabahrain pamoja na walimwengu kwa ujumla.

Utawala wa Bahrain umekuwa ukitoa hukumu za kidhalimu dhidi ya wananchi wanamapambano hasa wanazuoni na wasomi wa Kiislamu ambao wana nafasi katika jamii ya watu wa nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.

Ni kwa msingi huo ndio maana wananchi wa Bahrain wamekuwa wakiandamana nje ya nyumba ya Sheikh Qassim, mmoja kati ya viongozi wa harakati ya mwamko wa watu wa Bahrain. Maandamano hayo ya amani yanalenga kubainisha malalamiko kuhusu uamuzi wa kumpokonya uraia mwanazuoni huyo na pia kulalamikia hukumu zingine nyingi za mahakama za utawala ambazo zimekuwa zikikiuka wazi sheria za kimataifa.

Lengo jingine la Wabahrain katika kujumuika kila siku mbele ya nyumba ya Sheikh Issa Qassim ni kuhakikisha kuwa utawala wa kiimla wa Aal Khalifa hautekelezi njama za kumbaidisha au kumfukuza Bahrain Sheikh Qassim baada ya kumpokonya uraia wake.

Jeshi la Bahrain limeshadidisha ukandamizaji na ukatili dhidi ya raia huku idadi kubwa ya wanaharakati wakikamatwa na kuteswa sambamba na kupokonywa uraia. Watetezi wa haki za watu wa Bahrain wamebainisha wasiwasi wao kuhusu ukandamizaji na unyama unaotekelezwa na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya wananchi.

Utawala huo unazidi kuwapokonya Wabahrain haki zao sambamba na kuwakandamiza na kukiuka haki zao za binadamu kiasi kwamba utawala huo wa Aal Khalifa sasa umetambulika duniani kama utawala katili na dhalimu.Wabahrain waendeleza maandamano ya kumuunga mkono Sheikh Issa Qassima

Kutokana na hali hiyo, wananchi wa Bahrain nao wamekaidi amri ya wizara ya mambo ya ndani ya kupiga marufuku maandamano na mijumuiko katika mji mkuu Manama na maeneo mengine. Wananchi wa Bahrain wameonyesha azma yao imara ya kukabiliana na ukandamizaji wa utawala wa Aal Khalifa. Wanazuoni na wanafikra wa Kiislamu nchini humo nao pia wamesisitiza kuwa wananchi wa nchi hiyo katu hawataruhusu Sheikh Issa Qassima avunjiwe heshima. Aidha wameuonya utawala wa Bahrain kuhusu hatua yoyote yenye kumdhuru Sheikh Issa.

Matukio ya sasa Bahrain ni ishara kuwa, hali ya kisiasa nchini humo inazidi kuwa mbaya kutokana na ukosefu wa busara katika utawala wa Aal Khalifa.

Tangu mwaka 2011 Bahrain imekuwa uwanja wa maandamano ya wananchi dhidi ya utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa unaopata himaya ya Saudi Arabia na madola ya Kimagharibi hasa Uingereza na Marekani. Wabahrain wanataka kupewa uhuru, kuondolewa dhulma na ubaguzi na kupewa haki yao ya kimsingi ya kuchagua serikali wanayoitaka wao wenyewe badala ya kutawaliwa kwa mabavu na ukoo dhalimu wa Aal Khalifa.    

3461330


captcha