IQNA

Rais Rouhani atembelea maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHA

23:00 - November 05, 2016
Habari ID: 3470655
IQNA-Rais Hassan Rouhani Jumamosi ametembelea Maonyesho ya 22 ya Vyombo vya Habari hapa mjini Tehran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Rais Rouhania litembelea vibandaa kadhaa na kuzungumza na wawakilishi wa magazeti na mashirika ya habari.

Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho hayo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kuimarishwa umoja na mshikamano kwa ajili ya kuimarisha usalama na amani ya Mashariki ya Kati.

Amegusia hali ngumu inayotawala eneo la Magharibi mwa Asia kwa sasa na kusema kuwa, usalama wa eneo hili hauwezi kuimarishwa bila ya kuwepo mshikamano na umoja katika kupambana na magaidi na maadui.

Rais Rouhani amesema kuwa, matatizo ya sasa ya usalama ni ugaidi na fikra za kijahilia zinazopewa sura na rangi ya mafundisho ya dini na kwamba makundi yenye ufahamu usio sahihi na potofu kuhusu Uislamu yamekuwa yakiua Waislamu kwa kutumia fikra hizo.

Maonyesho ya 22 wa Vyombo vya Habari Iran yanafanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran na yataendelea hadi Ijumaa. Kuna zaidi ya vyombo vya habari 900 vinavyoshiriki yakiwemo magazeti, majarida, mashirika ya habari na mitandao ya habari.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) ni kati ya vyombo vya habari katika maonyesho hayo ambayo pia yatajumuisha mikutano, semina na warsha kadhaa. Halikadhalika kuna waandishi habari kutoka nchi za kigeni wanaoshiriki kama wageni waalikwa wa maonyesho hayo.Rais Rouhani atembelea maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHA

Rais Rouhani atembelea maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHA

Rais Rouhani atembelea maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHA
Rais Rouhani atembelea maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHARais Rouhani atembelea maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHARais Rouhani atembelea maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHA

3543449

captcha