IQNA

Israel yapiga marufuku adhana ya Sala ya Alfajiri mjini Quds

0:16 - November 06, 2016
1
Habari ID: 3470658
IQNA-Utawala wa Kizayuni wa Israel umepiga marufuku adhana ya Sala ya Alfajiri katika misikiti mitatu iliyo katika mji wa Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jumamosi, Novemba 5, utawala haramu wa Israel umetoa amri ya kusitishwa adhana ya Sala ya Alfajiri kutoka katika misikiti mitatu ya wilaya ya Abu Dis mjini Quds.

Taarifa zinasema mapema Jumamosi Alfajiri, askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel walihujumu misikiti ya Al-Rahman, Al-Taybeh and Al-Jamia katika wilaya ya Abu Dis na kuwafahamisha waadhini kuwa adhana ya Sala ya Alfajiri ni marufuku.

Ukandamizaji huo wa Israel umekuja siku moja baada ya walowezi wa Kizayuni wanaoishi katika kitongoji haramu cha Pisgat Zeev kulalamikia wakuu wa manispaa ya eneo hilo kuwa eti Adhana inasababisha kile walichodai kuwa ni kelele.

Kwa mujibu wa Bassam Bahr mkuu wa kamati ya Kipalestina huko Abu Dis, wanajeshi wa Israel waliingia katika wilaya hiyo kabla ya Sala ya Alfajiri Jumamosi. Amesema wanajeshi hao wa Israel pia waliwazuia Waislamu kuswali Sala ya Alfajiri katika msikiti wa Salah al Din. Bahr amelaani marufuku hiyo ya adhana na kusema utawala wa Kizayuni wa Israel unawahujumu Wapalestina katiak sekta zote za maisha yao.

Quds Tukufu ilikaliwa kwa mabavu na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku sita vya mwaka 1967. Kwa mujibu wa maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Quds ni eneo linalokaliwa kwa mabavu na hivyo Israel inapaswa kuondoka katika eneo hilo la Palestina bila masharti.

Utawala wa Israel unatekeleza mpango wa kujenga vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi hizo za Palestina. Aidha baada ya kupita zaidi ya miongo mitano, Waisraeli wanaendelea kuwazuia Wapalestina wakimbizi kurejea katika ardhi zao asili huko Quds na maeneo mengine ya Wapalestina.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa, ujenzi wa vitongozi unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina ni haramu, hata hivyo utawala huo ghasibu umeyadharaumaazimio hayo na kuamua kuendeleza upanuzi wa vitongoji hivyo.

3543498

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
amed
0
0
They ban the call prayer and now Allah shows them his power.
captcha