IQNA

Iran yalaani mauaji ya Waislamu katika maombolezo nchini Nigeria

18:07 - November 15, 2016
1
Habari ID: 3470677
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani mauaji ya Waislamu waliokuwa wakishiriki katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS kaskazini mwa Nigeria

Katika taarifa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi amebaini hayo na kuongeza kuwa, "ni jambo linalotia wasiwasi na lisilokubalika kuona kukaririwa mauaji ya kinyama ya Waislamu waliokuwa katika mjumuiko wa kidini na wa amani usio na tishio lololote wala ghasia."

Qassemi amewataka wakuu wa Nigeria wawe waangalifu kuhusu wanaozusha ghasia na mifarakano na wachukue hatua imara kuzuia kukaririwa tena jinai kama hizo.

Jana Waislamu wasiopungua 100 wa madhehebu ya Shia waliuawa nchini Nigeria kwa kupigwa risasi na jeshi la nchi hiyo.

Waislamu hao waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa walipokuwa katika mjumuiko huo wa kidini nje kidogo ya mji wa Kano ulioko kaskazini mwa Nigeria.

Wachambuzi wa mambo wanadokeza kuwa wanasema Jeshi la Nigeria linawashambulia na kuwaua kiholela Waislamu wa madhehebu ya Shia katika fremu ya kutekeleza sera za utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia.

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, Majlisi za siku ya Arubaini  hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.

3546260


Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
eddy manirambona
0
0
ni makosa ma islam kubaguwana kwa madhehebu yenu nakutukana wengine kama ni makafiri
captcha