IQNA

UNHCR

Jeshi la Myanmar linapanga mauaji ya kimbari Waislamu ya Rohingya

22:19 - November 25, 2016
3
Habari ID: 3470698
IQNA- Afisa wa Umoja wa Mataifa amesemajeshi la Myanmar linabeba dhima ya kampeni ya mauaji ya kimbari ya Waislamu wa Rohingya.

John McKissick, Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kusini mwa Bangladesh ametangaza kuwa, jeshi la Myanmar na viongozi wa serikali ya nchi hiyo wamekuwa wakiwalazimisha Waislamu wa jamii ya Rohingya kuyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani. Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa serikali ya Myanmar inatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu.

McKissick amesema Jeshi la Bangladesh limekuwa likuwaua wanaume, likiwachinja watoto pamoja na kuwanajisi wanawake sambamba na kuteketeza na kupora nyumba na kuwalazimisha watu kuvuka mto kuelekea nchi jirani ya Bangladesh.

Wakati huo huo, Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limeituhumu serikali ya Bangladesh kwamba, imekuwa ikiwarejesha Myanmar kwa nguvu Waislamu wa jamii ya Rohingya. Inaelezwa kuwa, kuna Waislamu takribani laki tano wa jamii ya Rohingya wanaoishi nchini Bangladesh kinyume  cha sheria.

Siku chache zilizopita mamia ya nyumba za Waislamu wa Myanmar zilichomwa moto magharibi mwa nchi hiyo sambamba na kuendelea ukandamizaji dhidi ya Waislamu hao.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu ambao idadi yaoni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu. Mabudhha wenye misimamo mikali Myanmar wanashirikiana na serikali katika kuwakandamiza, kuwatesa na kuwaua kiholela Waislamu.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia.

3548702

Imechapishwa: 3
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
ibrahim kimathi daresalam tanzania
0
0
mashirika ya haki za binadam mko wapi? na nyie bangladeshi hao si ndugu zenu ? nyinyi ndio majirani chondechonde wasaidieni. mnataka wakimbilie wapi? wahusika waliowauwa wakamatwe wachukuliwe hatua kali dhidi ya mauwaji ya kimbari. na ikibainika uyo rais wao ashitakiwe kwenye mahakama ya kimataifa dhidi ya mauwaji ya halaiki.

captcha