IQNA

Mwanamke Mwislamu hakumpa mkono rais wa Ujerumani, Je Waziri Msaudi?

18:54 - December 20, 2016
Habari ID: 3470751
IQNA- Mwanamke Mwislamu amekataa kumpa mkono Rais wa Ujerumani lakini Waziri wa Ulinzi wa Saudia amempa mkono mwanamke ambaye ni waziri wa ulinzi wa Ujerumani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hivi karibuni Rais wa Ujerumani Joachim Gauck alikumbwa na butwaa baada ya mwanamke Mwislamu mwenye kulinda imani yake alipokataa kumpa mkono alipokuwa katika ziara rasmi ya shule ya Theodor Heuss School karibu na mji wa Cologne. Mwanamke huyo Mwislamu aliyekuwa amevalia vazi la Kiislamu la Hijabu aliweka mkono wake kifuani na kutingisha kichwa chake kama ishara ya kumsalimu rais huyo badala ya kumpa mkono.

Kimsingi ni kuwa, mwanamke huyo hakumvunjia heshima Rais wa Ujerumani bali alitekeleza mafundisho ya Kiislamu ambayo yanaharamisha mwanamke Mwislamu kumpa mkono mwanaume ajnabi kama ambavyo mwanaume Mwislamu haruhusiwi kumpa mkono mwanamke ajnabi.

Hayo yanajiri wakati ambao siku chache zilizopita, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Bi. Ursula von der Leyen akiwa katika ziara rasmi Saudi Arabia alikataa kuvaa Hijabu kwa mujibu wa kanuni za nchi hiyo. Si hayo tu, bali waziri huyo alionekana Riyadh katika televisheni ya kitaifa akimpa mkono Waziri wa Ulinzi wa Saudia Mohammad bin Salman al Saud ambaye pia ni naibu mrithi wa kiti cha ufalme.Mwanamke Mwislamu hakumpa mkono rais wa Ujerumani, Je Waziri Msaudi?

Wasaudi ambao wanaipa Ujerumani mabilioni ya dola za kununua silaha walilazimika kutii matakwa ya waziri huyo ambaye pia alisema hakuna mwanamke katika ujumbe wake atayakelazimishwa kuvaa Hijabu.

Msimamo huo wa der Leyen unakuja siku chache baada ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kusema niqabu itapigwa marufuku nchini humo. Bin Salman ametetea hatua ya waziri huyo wa Ujerumani kukiuka sheria za Kiislamu.

3555115
captcha