IQNA

Bahrain yawaalika makuhani wanaotaka Wapalestina waangamizwe kwa umati

19:46 - December 30, 2016
Habari ID: 3470767
IQNA: Utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain umelaaniwa vikali kwa hatua yake ya kuwaalika makuhani wa Kizayuni wanaotaka Wapalestina waangamizwe kwa umati.

Zaidi ya wanaharakati 400 wa haki za binadamu nchini Bahrain wamelaani hatua ya Idara ya Biashara ya Utawala wa Aali Khalifa kushirikiana na Makuhani wenye misimamo ya kufurutu ada pamoja na Wazayuni kadhaa katika kuandaa sherehe ya Kizayuni yaHanukkah katika mji mkuu wa nchi hiyo, Manama. Aidha wanaharakati hao wamelaani Bahrain kwa kujikurubisha na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa, wanaharakati hao wametaka wafanyabiashara wote Wabahrain walioshiriki katika sherehe hiyo ya Kizayuni kuadhibiwa. Huku wakilaani kufanyika sherehe hiyo ya Kizayuni mjini Manama, wametangaza kufungamana kwao na mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza udharura wa kuundwa taifa huru la Palestina mji wake mkuu ukiwa ni Quds Tukufu.

Makuhani walioshiriki katika shehrehe hioyo mjini Manama Jumamosi ni kutoka pote la Chabad la Mayahudi wa Kizayuni wenye misimamo mikali na ambao wanaamini kuwa Wapalestina wanapaswa kuangamizwa kwa umati. Ujumbe wa makuhani hao ulifika Bahrain kwa mwaliko rasmi wa mfalme.

Maulamaa nchini Bahrain wamelaani juhudi za utawala wa nchi hiyo za kuweka uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hivi sasa kuna nchi kadhaa za Kiarabu ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja au wa siri na utawala wa Kizayuni wa Israel. Nchi za Kiarabu zenye uhusiano rasmi na Israel ni Jordan na Misri huku nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi hususan Saudi Arabia, Qatar, Bahrain na Imarati zikiwa na uhusiano wa siri na utawala haramu wa Israel. Mwaka 2015, utawala wa Kizayuni ulikuwa mwenyeji wa maafisa wa Saudi Arabia kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi huko Haifa.

Uhusiano huo wa tawala za Kiarabu na Israel ni usaliti wa wazi kwa Wapalaestina na Waislamu duniani kwa kuzingatia kuwa Israel inakali kwa mabavu Msikiti wa Al Aqsa ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu na sehemu ya tatu kwa utakatifu katika Uislamu.

3557827

captcha