IQNA

Qur'ani Tukufu yatarjumiwa kwa lugha ya Kiyao ya Malawi+PICHA

11:59 - January 01, 2017
Habari ID: 3470771
IQNA-Qur'ani Tukufu iliyotarjumiwa kwa lugha ya Kiyao imezinduliwa ncchini Malawi siku ya Jumamosi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Qur'ani hiyo imezinduliwa katika kwa pamoja na Jumuiya ya Waislamu Malawi (MAM) na Baraza la Iftaa la Mualmaa la Malawi katika mji wa Mangochi kusini mwa nchi hiyo.

Sheikh Muhammad Abdul-Hamid Silika ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Iftaa la Maulamaa wa Malawi amechukua muda wa miaka 10 kuitarjumu Qur'ani kwa Kiyao kutoka lugha ya Kiarabu.

Aidha tarjuma hiyo imepitiwa kwa muda wa miezi sita na jopo la maulamaa 14 na nakala 20,000 za kwanza zimechapishwa kwa himaya ya Jumuiya ya Misaada ya Dubai.

Rais wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi amekuwa mtu kwa kwanza kununua Qur'ani kwa lugha ya Yao ambapo amenununua nakala 200 na kuzikabidhi kwa wanawake waliohudhuria sherehe za uzinduzi huo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, kaimu mwenyekiti wa chama cha Peoples Part Uladi Mussa amesema tarjuma hiyo itawasaidia Waislamu ambao lugha yao asili ni Kiyao kufahamu Qur'ani Tukufu na Uislamu kikamilifu.

"Baina ya asilimia 60-70 ya Waislamu wa Malawi ni Wayao na hivyo ni muhimu kwa Qur'ani Tukufu kutarjumiwa kwa lugha wanayoifahamu kwa urahisi. Ni fahari kubwa kuwa imeweza kutarjumiwa baada ya tarjuma nyigine ya Chichewa miaka kadhaa iliyopita.," amesema Mussa.

Mwanasiasa hiyo pia ametoa wito kwa Wamalawi kuweka kando tafauti zai za kidini na waelekeze nguvu zao katika ujenzi wa nchi huku akiwataka Waislamu na wafuasi wa dini nyinginezo kuwekeza zaidi katika elimu.

Wayao ni kabila la Kibantu kutoka eneo la karibu na Ziwa Nyasa barani Afrika ambapo ina wazungumzaji takribani milioni mbili nchini Malawi na nusu milioni Tanzania katika mikoa ya Mtwara na Ruvuma na nusu mwilini wengine nchini Msumbiji.

Aghalabu ya Wayao ni waumini wa dini ya Uislamu na miongoni mwao waliopata umaarufu mkubwa ni pamoja na marais wawili wa zamani wa Malawi Bakili Muruzi pamoja na Joyce Banda.

Qur'ani Tukufu yatarjumiwa kwa lugha ya Yao ya Malawi+PICHAQur'ani Tukufu yatarjumiwa kwa lugha ya Yao ya Malawi+PICHA

Qur'ani Tukufu yatarjumiwa kwa lugha ya Yao ya Malawi+PICHA

Qur'ani Tukufu yatarjumiwa kwa lugha ya Yao ya Malawi+PICHA

3558323

captcha