IQNA

Mashindano ya Qur'ani nchini Japan

12:05 - January 03, 2017
Habari ID: 3470778
IQNA-Mashindano ya Qur'ani ya Waislamu wa Japan yamefanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tokyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yaliyokuwa na anuani ya, "Mashindano ya Qur'ani ya Kote Japan", yalikuwa yanafanyika kwa mwaka wa 17 sasa na yalifanyika katika Kituo cha Kiarabu-Kiislamu eneo la Hiroo, Tokyo kuanzua Disemba 30-31.

Mashindano hayo yameandaliwa na Waqfu wa Kiislamu Japan kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani.

Mashindano hayo yameandaliwa kwa ajili ya makundi mawili ya vijana na watu wa zama katika ambayo yalikuwa na vitengo vya wanawake na wanaume.

Aidha katika kategoria za kuhifadhi kulikuwa na mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 5,2,1 na nusu juzuu.

Mkurugenzi wa Kituo cha Kiarabu-Kiislamu cha Japan Nasir al Naeem, mkurugenzi wa Waqfu wa Kiislamu Japan Sheikh Aqil Sediqi na viongozi wengine wa jamii ya Waislamu japan ni kati ya walioshiriki katika sherehe za kufunga mashindano hayo.

Washindi wa kila kitengo walitunukiwa zawadi ya safari ya Ummrah iliyogharamiwa kikamilifu.

Aghalabu ya wakaazi wa milioni 123 nchini Japan wanafuata dini za Kishinto na Kibuddha huku Waislamu nchini humo wakikadiriwa kuwa takribani 70,000 ambapo miongoni mwao Waislamu ambao kiasili ni Wajapani wakiwa 10,000 na waliosalia ni raia wa kigeni.

3461842/
captcha