IQNA

Algeria yasambaratisha mtandao wa kijasusi wa Wazayuni

13:40 - January 15, 2017
Habari ID: 3470795
IQNA: Algeria imesambaratisha mtandao wa kijasusi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.
Algeria yasambaratisha mtandao wa kijasusi wa Wazayuni

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanachama 10 wa mtandao huo wa kigaidi walikamatwa Ijumaa katika mkoa wa Ghardaia wakiwa wanatekeleza njama za kuibua ghasia na machafuko.

Majasusi waliokamatwa wanaripotiwa kuwa na uraia wa Libya, Mali, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Kenya na hivi sasa wanashikiliwa na maafisa wa usalama.

Gazeti la el-Bilad limeandika kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa waliokamatwa walikuwa waskishirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mtandao huo wa kigaidi ulikuwa ukitumia suhulza za kisasa za mawasiliano kupeleleza mashirika ya usalama wa taifa nchini Algeria.

Katika miaka ya hivi karibuni, nchi kadhaa za Kiafrika zimewakamata na kuwafunga jela watu kadhaa ambao wamekuwa wakiufanyia ujasusi utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mwaka 2015 Misri ilimfunga jela raia wan chi hiyo ambaye alipatikana na hatia ya kuufanyia ujasusi utawala haramu wa Israel katika eneo linalkumbwa na msukosuko la Rais ya Sinai.

Mapmea mwezi huu pia, Tunisia iliutuhumu utawala haramu wa Israel kuwa ulihusika katika kumuua mhandisi wa ndege, Mohamed Zaouari alieykuwa akisaidia harakati ya mapambano ya Kislamu ya Palestina, Hamas, katika kuunda ndege zisizo na rubaini au drone.

http://iqna.ir/fa/news/3562413

Kishikizo: iqna algeria wazayuni
captcha