IQNA

Rais Hassan Rouhani

Ayatullah Rafsanjani alikuwa nguzo imara ya Kiongozi Muadhamu

7:57 - January 16, 2017
Habari ID: 3470798
IQNA- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kuaga dunia Ayatullah Hashemi Rafsanjani, ni msiba mkubwa ambao umepelekea Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kupoteza tegemeo lake kubwa."

Ayatullah Rafsanjani alikuwa nguzo imara ya Kiongozi Muadhamu
Rais Hassan Rouhani Rouhani ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran katika kikao cha baraza la mawaziri na aliongeza kuwa, Ayatullah Rafsanjani alikuwa msaidizi imara wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Aidha amesema huduma za Ayatullah Rafsanjani kwa Uislamu, Mapinduzi ya Kiislamu na taifa la Iran ni sababu ya kimsingi iliyopelekea idadi kubwa ya watu kujitokeza katika mazishi yake.Hassan Rouhani aidha ametoa wito kwa maafisa wa serikali na wale wote waliompenda marehemu Ayatullah Hashemi Rafsanjani kujitahidi zaidi kuwahudumiwa wananchi sambamba na kumuunga mkono Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah Rafsanjani aliaga dunia Jumapili iliyopita baada ya umri mrefu wa jihadi na jitihada zisizo na kikomo kwa ajili ya Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah Rafsanjani, ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 82 kutokana na mshtuko wa moyo, alizikwa Jumanne katika Haram Takatifu ya Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wakati huo huo khitma ya siku ya saba ya marehemu Ayatullah Hashemi Rafsanjani ilimefanyika katika Haram Takatifu ya Imam Khomeini MA na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu wa matabaka mbali mbali. Ayatullah Rafsanjani alikuwa mwenye azma imara katika harakati ya Mapambano ya Kiislamu yaliyoongozwa na Imam Khomeini MA.

Kati ya nyadhifa ambazo Ayatullah Rafsanjani aliwahi kushika baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, Kaimu Amri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Ulinzi wa Kitaifa na nafasi aliyoishika hadi kifo chake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu.

3563076


captcha