IQNA

Msikiti mwingine wateketezwa moto Marekani, mara hii Texas

19:45 - January 29, 2017
1
Habari ID: 3470820
IQNA: Chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu zinaendelea kushika kasi Marekani huku msikiti mwingine ukiteketezwa moto katika katika jimbo la Texas.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mapema Jumamosi, moto uliteketeza kikamilifu Kituo cha Kiislamu cha Victoria ambacho hutumika kama msikiti wa wakaazi wa mji huo.

Mkuu wa kituo hicho cha Kiislamu, Shahid Hashmi amesema: "Ni masikitiko makubwa kusimama hapa na kuona jengo lote likiwa limeteketea na kuporomoka, moto ulikuwa mkubwa sana."

Mkuu wa zimamoto katika mji wa Victoria, Texas, Tom Legler anasema amelazimika kuomba msaada wa Idara Kuu ya Zimamoto Texas ili kubaini chanzo cha moto huo. Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusu kitendo hicho cha jinai ambacho ni muendelezo wa hujuma zinazowalenga Waislamu na maeneo yao ya ibada kote Marekani. Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika kitendo hicho cha jinai ambacho kimelenga jengo hilo lililojengwa mwaka 2000.Msikiti huo umeteketezwa moto siku chache tu baada ya wezi kuuhujumu na kuiba vifaa vya kielektroniki. Miaka michache nyuma, kituo cha Kiislamu cha Victoria kinachojumuisha msikiti huo wa Texas kilishambuliwa mara kadhaa na watu wenye misimamo ya kibaguzi.

Shambulio dhidi ya msikiti huo ni hujuma ya pili kulenga msikiti katika jimbo hilo katika kipindi cha mwezi huu wa Januari.

Tarehe 7 mwezi huu msikiti uliokuwa ukiendelea kujengwa karibu na eneo la Mto Travis katika mji wa Austin ulichomwa moto na kuteketezwa kikamilifu.

Katikati ya mwezi huu wa Januari pia watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wameuteketeza moto msikiti katika mji wa Bellevue, jimboni Washington nchini Marekani.Msikiti mwingine watektezwa moto Marekani, mara hii Texas

Moto huo uliteketeza Kituo cha Kiislamu cha Eastside (ICOE) ambacho pia kinajulikana kama Bellevue Masjid au Bellevue Mosque mapema Jumamosi asubuhi. Kituo hicho cha Kiislamu kimekuwa kikiwahudumia Waislamu wa eneo hilo kwa muda wa miaka 14 sasa. Ingawa hakuna mtu yeyeote aliyejeruhiwa katika mtoto huo lakini nusu ya jengo hilo la Waislamu liliharibiwa kabisa katika moto huo. Kumeshuhudiwa wimbi la hujuma dhidi ya Waislamu kote Marekani baada ya Donald Trump kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais mwezi Novemba mwaka jana. Chuki hizo zimeshika kasi zaidi baada ya Trump kuapishwa tarehe 20 Januari. Siku ya Ijumaa Trump alitekeelza ahadi ya kampeni yake ya uchaguzi na kupiga marufuku raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia Markeani, hatua ambayo imelalamikia na wengi na pia imekuwa ni kichochezi kwa wenye chuki kuwahujumu Waislamu.

Kwa mujibu Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR), ambalo hutetea haki za Waislamu, mbali na misikiti na vituo vya Kiislamu kushambuliwa pia wanawake na watoto Waislamu wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

http://iqna.ir/en/news/3462063
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
KassImu
0
0
Allah yupo pamoja na wao atawasaidia waislam ila wajue hawawezi kupambana na uislam mungu wape gharika marekani
captcha