IQNA

Gaidi mfuasi wa Trump ndiye aliyewaua Waislamu msikitini Canada

10:43 - February 01, 2017
Habari ID: 3470827
IQNA: Gaidi Mkristo aliyewaua Waislamu sita katika msikiti mmoja nchini Canada amebainika kuwa mfuasi wa Rais Donald Trump wa Marekani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gaidi huyo ametambuliwa kuwa Alexandre Bissonnette mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni Mkristo mwenye misimamo mikali ya kibaguzi ya mrengo wa kulia mbali na kuwa mkereketwa wa Trump.

Gaidi huyo, akitumia bunduki aina ya AK47 aliwafyatulia risasi Waislamu waliokuwa katika msikiti wa Kituo cha Kiutamaduni cha Quebec, wakati wa Sala ya Ishaa Jumapili saa mbili usiku kwa wakati wa Quebec ( 0100 GMT Jumatatu).

Katika mitazamo yake aliyochapisha katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Bissonnette amekuwa akibainisha wazi kuwa anaunga mkono misimamo ya chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) na Waislamu ya Trump. Halikadhalika ni mfuasi wa vuguvugu la mrengo la mrengo wa kulia la Parti Quebecois ambalo linataka eneo la Quebec lijitenge na Canada.Gaidi mfuasi wa Trump ndiye aliyewaua Waislamu msikitini Canada

Waislamu waliouawa na gaidi Mkristo walipokuwa wakiswali ndani ya msikiti nchini Canada

Halikadhalika, katika kurasa wake wa Facebook kuwa gaidi huyo Mkristo amesema anafurahishwa sana na misimamo yaMarine Le Pen, mwanasiasa wa mrengo wa kulia wa Ufaransa ambaye amekuwa akipigia debe sera za chuki dhidi ya Waislamu na wahamiaji nchini humo.

Bissonnette ambaye ni Mzungu anajinadi kuwa ni Mkristo mwenye katika mstari wa mbele wa vita vya msalaba huku akibainisha mapenzi yake kwa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.

3462093
captcha