IQNA

Ubaguzi wa Trump

Mtoto Muirani wa miaka mitano afungwa pingu Marekani+Video

22:58 - February 02, 2017
1
Habari ID: 3470830
IQNA: Polisi nchini Marekani wamemtia mbaroni na kumfunga pingu mtoto wa miaka mitano Muirani katika hatua ya ubaguzi iliyojiri huko Uwanja wa Ndege wa Jimbo la Virginia.
Mtoto Muirani  wa miaka mitano afungwa pingu Marekani+VideoKwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, siku ya Jumanne, mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano alikamatwa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Dulles mjini Virginia karibu na mji mkuu wa Marekani Washington DC.

Mtoto huyo alizuiliwa kwa masaa kadhaa katika uwanja huo kufuatia amri ya kibaguzi ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwapiga marufuku raia wa nchi saba za Kiislamu, ikiwemo Iran kuingia Marekani.

Polisi katika jimbo la Virginia walimkamata mtoto huyo Muirani ambaye pia ana uraia wa Marekani na kumfunga pingu kwa masaa kadhaa katika uwanja huo wa ndege. Taarifa zinasema mama ya huyo mtoto ni mzaliwa wa Maryland Marekani na ana asili ya Iran.

Mtoto huyo alikamatwa na kusailiwa kwa masaa kadhaa lakini polisi hawakutoa maelezo kuhusu tukio hilo. Mtoto huyo, ambaye alikuwa amewasili Marekani akitokea Iran akiwa ameandamana na familia nyingine, alikamatwa katika siku ya kuadhmisha kuzaliwa kwake. Lakini pamoja na hayo msemaji wa Rais Donald Trump, Sean Spicer, ametetea kitendo hicho cha polisi kumakamata na kumfunga pingu mtoto wa miaka mitano. Spicer amedai kuwa: "Kudhani kuwa umri au jinsia ya mtu itafanya asiwe tishio ni makosa."

Taswira za video zinaonyesha mama yake mtoto huyo akiwa anatokwa na machozi wakati akisuburi mwanae aachilwe huru na maafisa wa polisi. Baada ya mtoto huyo kuachiliwa huru, mama yake alimkumbatia huku akitokwa na machozi ya furaha. Mwanamke huyo hakuzungumza na waandishi habari baada ya tukio hilo.

Mkasa huo unakuja huku kukiwa na hasira na ghadabu kote duniani kufuatia hatua ya Trump kuwapiga marufuku raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia nchini humo. Nchi hizo ambazo raia wake wamepigwa marufuku kuingia Marekani ni pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Syria, Iraq, Yemen, Libya , Sudan na Somalia.

Waandamanaji wamekusanyika katika vijanwa vya ndege kote Marekani, ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Dulles, kuonyesha uungaji mkono wao kwa wakimbizi na raia wa nchi ambazo zimelengwa na marufuku hiyo.

Tizama video ya tukio hapo chini.

3569802


Ubaguzi wa Trump: Mtoto Muirani wa miaka mitano afungwa pingu Marekani


Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Hassan
0
0
Makala nzuri
captcha