IQNA

Wanawake wawakilishi wa Iran katika mashindano ya Qur'ani wachaguliwa

13:25 - February 22, 2017
Habari ID: 3470863
IQNA-Iran imechagua wanawake watakaoiwakilisha nchi hii katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yatakayofanyika maeneo mbali mbali duniani mwaka huu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanawake na wasichana hao wamechaguliwa katika mashindano ya mchujo yaliyoandaliwa na Kamati ya Kuwatuma Wasomaji Qur'ani katika Mashindano ya Kimataifa. Baada ya mchujo huo Bi. Zahra Qurbani ametajwa kuwa wawakilishi wa Iran katika mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Jordan.Wanawake wawakilishi wa Iran katika mashindano ya Qur'ani wachaguliwa

Aidha Bi. Zeinab Mohammadnejad atawakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yatakayofanyika mjini Tehran mwezi Aprili.Wanawake wawakilishi wa Iran katika mashindano ya Qur'ani wachaguliwa

Mashindano hayo ya Qur'ani ya wanawake mjini Tehran yatafanyika samamba na Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3462268

captcha