IQNA

Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kufanyika Mwezi wa Ramadhani

18:47 - February 27, 2017
Habari ID: 3470870
IQNA-Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yamepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hujjatul Islam Muhammad Ridha Hishmatu Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran, kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma maonyesho hayo yatafanyika katika ukumbi huo wa Sala. Amesema tayari mipango imeshaanza kufanikisha maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran na kuleta pamoja mashirika na watu wanaojihusisha na kazi zinazohusiana na Qur'ani Tukufu.

Lengo kuu la maonyesho ya Qur'ani katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kustawisha ufahamu wa Qur'ani na pia kueneza harakati za Qur'ani kitaifa na kimataifa.

3462302
captcha