IQNA

Misikiti 10 Mikubwa Bora Nchini Russia


المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
1. Msikiti wa Nurda Kamal uko Norilsk kaskazini mwa Siberia na ulifunguliwa mwaka 1998. Msikiti huo uko katika Kitabu cha Guinness cha Rekodi za Dunia kwa kuwa msikiti ulio eneo la kaskazini zaidi duniani.

المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
2. Msikiti wa Jamia wa Moscow ni msikiti mkubwa zaidi barani Ulaya ambao una ghorofa sita na minara yenye urefu wa mita 79 ambayo ni mirefu zaidi Ulaya.

المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
3. Msikiti wa Samawati ambao uliasisiwa mwaka 1910 katika kisiwa cha Petrogradsky. Huu ni msikiti pekee Ulaya uliojengwa katika kisiwa kilicho katika mto.

المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
4. Msikiti wa Sultan Delimakhanov ni msikiti mkubwa zaidi ulio kijijini barani Ulaya na uko katika kijiji cha Dzhalka katika jimbo la Chehenia. Huu ni msikiti uliojengwa kumuenzi Sultan Delimkhanov afisa wa kijiji aliyeuawa muongo wa 1990 na unaweza kutumiwa wakati moja na waumini 5,000
 


المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
5. Msikiti wa Jamia wa Derbent, jimbo la Daghestan ulijengwa kati ya mwaka 733 na 734 Miladia na umetajwa kuwa msikiti mkongwe Zaidi Raussia. Msikiti huu uko katika orodha ya UNESCO ya turathi za dunia.

المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
 
6. Msikiti wa Jamia wa Makhachkala katika jimbo la Daghestan ulijengwa mwaka 1997 kupitia ufadhili wa moja ya familia tajiri zaidi


المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
7. Msikiti wa Kul Sharif wa Kazan ulijengwa sehemu ilimokuwa hekalu adhimu ya Ivan Groznya iliyoharibiwa katika kampeni zake za kivita mwaka 1547-52. Msikiti huo una minara sita yenye urefu wa mita 55 na uko katika orodha ya UNESCO ya turathi za dunia.

المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
8. Msikiti wa Jamia wa Madrasa Lala-Tulip ulijengwa mwaka 1990-98 kwa usanifu majengo wa kisasa na una minara pacha yenye urefu wa mita 53.
 


المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا
9. Msikiti wa Bulgar huko mjini Kazan katika jimbo la Tatarstan na ni msikiti pekee Russia ambao kuta zake zote zina rangi nyeupe. Msikiti huu pia una nakala kubwa zaidi ya Qur'ani duniani.

المساجد العشرة الأكثر تميزاً في روسيا

10. Msikiti wa Ahmad Kadyrov katika jimbo la Chehnia umetajwa kuwa Moyo wa Chechenia na unashabihiana sana na ule Msikiti wa Samawati wa Istanbul. Msikiti huo ndio msikiti pekee Russia ambao taswira zake za video zinarushwa hewani masaa 24 kwa siku