IQNA

Mwanamke Mwislamu mwenye Hijabu kukimbia mbio za marathon Boston

16:41 - March 13, 2017
Habari ID: 3470891
IQNA: Kwa mara ya kwanza katika historia ya mbio maarufu za marathon za Boston, Marekani, mwanamke Mwislamu atashiriki akiwa amevaa Hijabu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Rahaf Khatib mwanariadha mwanamke Mwislamu mwenye umri wa miaka 33 atashiriki katika mbio hizo za marathon katika timu maalumu ya wanawake ya kuadhimisha mwaka wa 50 tokea mwanamke wa kwanza aliposhiriki katika mashindano hayo mwaka 1967.

Akizungumza na shirika la habari la NBC, Khatib amesema: "Kuna umuhimu kwani mimi kushiriki katika timu ya wanariadaha wanawake, na ninafikiri kuwa jambo hili linaashiria hadhi waliyopata wanawake na walikotoka."

Ameongeza kuwa, "nataka pia kuthibitisha kuwa mwanamke Mwislamu anaweza kukimbia mbio za marathon." Bi. Khatib ambaye asili yake ni Damascus, Syria alihamia Marekani muongo wa 1980 na anaishi Michigan na mume wake pamoja na watoto watatu.

/3462408

captcha