IQNA

Mahakama ya Ulaya yalaaniwa kwa kupiga marufuku Hijabu

16:19 - March 16, 2017
Habari ID: 3470897
IQNA-Mahakama ya Uadilifu ya Ulaya imekosolewa vikali na Waislamu kwa kutoa hukumu kuwa waajiri barani humo wanaweza kuwazuia wafanyakazi wa kike Waislamu kuvaa hijabu kazini.

Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani limekosoa vikali hukumu hiyo likisema inakiuka haki za kimsingi ambazo zimeainishwa katika mikataba muhimu ya Ulaya kuhusu haki za binadamu.

Kwa upande wake, Bekir Altas, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Milli Gorus, inayowakutanisha pamoja Waislamu wenye asili ya Uturuki huko Ujerumani, amelaani hukumu ya mahakama hiyo.

Altas amebainisha wasi wasi wake kuwa, wanawake Waislamu wanaweza kutengwa zaidi katika soko la ajira na hivyo, kupoteza fursa ya kujitegemea kiuchumi. "Hili ni jambo lisilokubalika. Wanasaisa wanapaswa kuchukua hatau za dharura katika Bunge la Ulaya kutunga sharia za kuzuia ubaguzi," ameongeza.

Siku ya Jumanne, Mahakama ya Haki ya Ulaya (ECJ) yenye makao yake huko Luxembourg iliyopita ilipasisha marufuku ya vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu.

Wakati huo huo wimbi la wakimbizi kueleka katika nchi za Ulaya ambao wengi wao ni Waislamu, limezidisha chuki na propaganda chafu dhidi ya wageni na Waislamu barani humo. Wimbi hilo linaambatana na hujuma kubwa ya kipropaganda ya makundi yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia ambayo yanawalenga hata Waislamu waliozaliwa na kukulia katika nchi za Magharibi.

La kusikitisha zaidi ni kuwa, kwa sasa hakuna mwanga wa matumaini ya kupatikana faraja kwa Waislamu huko katika nchi za Magharibi na hapana shaka kuwa, hukumu ya Mahakaya ya Haki ya Ulaya (ECJ) itachochea zaidi hujuma, mashinikizo na ubaguzi dhidi ya Waislamu katika nchi za bara hilo ambazo zimekuwa zikijinadi kuwa eti ni watetezi wa demokrasia na haki za binadamu. Hivi sasa imebainika kuwa nchi za Ulaya zinatenda kinyume ya zinavyosema.

3462429/
captcha