IQNA

Nchi 40 kushiriki mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Misri

23:30 - March 22, 2017
Habari ID: 3470904
TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Awqaf Misri imesema nchi 40 zimetangaza kuwa tayari kushiriki katika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya al-Bilad, washiriki 52 kutoka nchi 40 wanatazamiwa kushiriki katika mashindano ya 24 ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Misri.

Mashindano hayo yanatazamiwa kufanyika Aprili 8-11 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Taarifa hiyo imesema mashindano hayo yanatazamiwa kufunguliwa rasmi katika sherehe zitakazohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu akiwemo Waziri wa Awqaf Sheikh Mohammad Mukhtar Gomaa pamoja na masutadhi bingwa wa Qur’ani nchini humo.

Wizara ya Awqaf Misri inasema moja ya malengo muhimu ya mashindano hayo ni kustawisha kiwango cha kuhifadhi Qur’ani miongoni mwa vijana.

3585443

captcha