IQNA

HRW: Waislamu India wanauawa kwa ajili ya kuchinja ng'ombe

19:40 - April 28, 2017
Habari ID: 3470957
TEHRAN (IQNA)- Shirika la kutetea hakiza binadamu la Human Rights Watch (HRW) limelaani vikali magenge ya wafuasi wa dini ya Kihindu wanaowahujumu na kuwaua Waislamu India kwa sababu tu ya kununua, kuuza au kichinja ng'ombe kwa ajili ya nyama.
HRW: Waislamu India wanauawa kwa ajili ya kuchinja ng'ombe

Katika taarifa Ijumaa, HRW imeitaka serikali ya India ichukue hatua kuzuia mauaji yanaotekelzwa na Wahindu dhidi ya Waislamu kwa ajili tu wanaochinja ng'ombe.

HRW imelaani vikali magenge ya wafuasi wa dini ya Kihindu wanaodai kuwa eti ni walinzi wa ng'ombe ambao wanawahujumu na kuwaua Waislamu na watu wa daraja la chini katika jamii kwa sababu tu wanaouza, kununua au kichinja ng'ombe kwa ajili ya nyama.

HRW inasema tokea Waziri Mkuu Narendra Modi aingie madarakani mwaka 2015 hadi sasa, karibu Waislamu 10 wameuawa na magenge ya Wahindu wanaowashambulia kwa sababu tu ya kuchinja ng'ombe kwa ajili ya nyama. Ingawa Modi amelaani hujuma hizo, lakini serikali yake inalaumiwa kwa kutochukua hatua za kutosha kuzuia mauaji ya Waislamu. Magenge ya Wahindu wenye misimamo mikali wanafungamana na chama tawala cha Bharatiya Janata ndio wanaowashambulia Waislamu . Wahindu wanamtazama ng'ombe kama mnyama mtakatifu na wanapinga kuchinjwa kwake kwa ajili ya nyama.

Wakati huo huo Sheikh Mirwaiz Umar Farooq, mmoja ya wanaopigania kujitenga eneo la Kashmir na India ameituhumu serikali ya India kwa kuyapa uhalali magenge ya Wahindu wanaowaua Waislamu. Amesema badala ya serikali ya India kuwasilisha sheria za kuwalinda waliowachache nchini humo , hasa Waisalmu, wanaohujumiwa na kuuawa na Wahindi wenye misimamo ya kufurut ada, hivi sasa serikali hiyo inapendekeza sheria za kuifanya ng'ombe iwe na umuhimu kuliko raia Waislamu nchini humo.

/3593871

captcha