IQNA

Mashindano ya Qur'ani Uganda katika Mwezi wa Ramadhani

11:55 - May 14, 2017
Habari ID: 3470980
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu yatafanyika nchini Uganda katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa ushirikiano wa Ofisi ya Utamaduni ya Iran na Radio Bilal nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bw. Musa Mugerwa mkurugenzi wa radio ya Kiislamu ya Bilal amemtembelea Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Kampala Bw. Ali Bakhtiari ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu kushirikiana katika kuandaa Mashindano ya Qur'ani Tukufu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika mkutano huo Mugerwa ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono harakati kadhaa za kidini na za Qur'ani katika Radio Bilal na ameomba ushirikiano huo uendelee katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema Madrassha zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni mara mbili zaidi ya mwaka jana na kwa msingi huo amesisitiza kuhusu kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili.

Kwa upande wake Bakhtiari ameishukuru Radio Bilal kwa kuwa na vipindi mbali mbali vya Kiislamu hasa kuandaa mashindano ya Qur'ani baina ya Madrassah za Uganda katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha amesema Radio Bilal ambayo ni radio rasmi ya Waislamu wa Uganda inayosimamiwa na Baraza Kuu la Waislamu Uganda inapaswa kuwa na kiwango bora cha vipindi ili kukidhi mahitaji ya Waislamu nchini humo. Aidha  kwa kuzingatia kuwepo wafuasi wa dini nyinginezo Uganda, ametoa wito kwa Radio Bilal kuandaa vipindi vyenye kuleta maelewano baina ya wafuasi wa dini zote sambamba na kuleta mshikamano baina ya madhehebu za Kiislamu na watu wa makabila mbali mbali. Halikadhalika amesema anaunga mkono jitihada za Radio Bilal kuandaa mashindano ya Qur'ani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na vipindi vingine vya Kiislamu na malezi ya Kiislamu.

3599140
captcha