IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Afrika Mashariki yafanyika Djibouti

10:52 - June 07, 2017
Habari ID: 3471011
TEHRAN-(IQNA)-Mashindano ya 18 ya Kieneo ya Qur'ani Tukufu yameanza Jumapili nchini Djibouti.

TEHRAN-(IQNA)-Mashindano ya 18 ya Kieneo ya Qur'ani Tukufu yameanza Jumapili nchini Djibouti.

Taarifa zinasema mashindano hayo yana washiriki kutoka Somalia, Sudan, Kenya, Tanzania, Visiwa vya Comoro, Uganda, Djibouti na pia Yemen.

Washiriki wanashindana katika vitengo vitatu vya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, kuhifadhi juzuu 20 na kuhifadhi juzuu 10 na wanatakiwa kuzingatia sheria za Tarteel na Tajweed. Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na huwaleta pamoja washiriki kutoka nchi hizo za mashariki mwa Afrika pamoja na Yemen. Wizara ya Masuala ya Kiislamu Djibouti imekuwa ikiandaa mashindano hayo tokea mwaka 1999. Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibuoti anatazamiwa kushiriki katika sherehe za kuwatunuku zawadi washindi wa mashindano hayo.

Djibouti ni nchi ndogo iliyo katika Pembe ya Afrika ambayo asilimia 94 ya wakaazi wake takribani 800,000 ni Waislamu. Nchi hiyo iliyokoloniwa na Ufaransa na ambayo pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu iko katika eneo muhimu la kistratijia la Lango Bahari la Babul Mandeb.


3606520
captcha