IQNA

Wenye ulemavu wa macho Malaysia wahifadhi Qur'ani kutumia Braille

9:19 - June 10, 2017
Habari ID: 3471015
TEHRAN (IQNA)-Jamii ndogo wa wanafunzi wenye ulemavu wa macho Malaysia wanajitahidi kuhifadhi Qur'ani kikamilifu kwa kutegemea misahafu iliyoandikwa kwa maandishi ya nukta nundu au Braille.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani wanafunzi nane katika jimbo la kati la Selangor nchini Malaysia wanajitahidi kuhifadhi Qur'ani Tukufu huku wakisoma kila ukurasa mara 40.

Wanafunzi hao wote ambao walizaliwa wakiwa na ulemavu wa macho ni miongoni mwa wanafunzi 1,000 wa Chuo cha Darul Qur'an wanaojitahidi kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Wanatumia nakala ya Qur'ani ya Braille ambayo imechapishwa Malaysia na iliyo na jildi sita.

Mwalimu wa Qur'ani Ahmad Qusairi Mat Zizi ambaye pia ana ulemavu wa macho anasema: "Wanapaswa kuhifadhi kurasa moja au mbili kwa siku na kwa kawaida husoma ukurasa moja mara 30 hadi 40 ili kuweza kuhifadhi."

Wanafunzi hao wana umri wa kati ya miaka 19-21 na wako katika kozi ya miaka mine ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, kusoma Kiarabu na masomo mengine ya Kiislamu. Baada ya kumaliza kozi hiyo wanaweza kuingia katika chuo kikuu kwa ajili ya masomo ya Kiislamu.

Siku chache zilizopita, Waziri Mkuu wa Malaysia Ahmad Zahid Hamidi alisema anatumai kuwa ifikapo mwaka 2050, nchi hiyo itakuwa na watu 125,000 waliohifadhi Qur'ani kikamilifu. Amesema hatua hiyo itakuwa muhimu katika kuleta maelewano na ustawi nchini humo.

3607535

captcha