IQNA

Shule Afrika Kusini yakosolewa kuanzisha kitambulisho cha wenye kuvaa Hijabu

14:24 - June 11, 2017
Habari ID: 3471016
TEHRAN (IQNA)-Shule moja nchini Afrika Kusini imekosolewa kwa kuanzisha vitambulisho maalumu kwa wanafunzi wa kike Waislamu wanaotakiwa kuvaa Hjabu.

Kufautia malalamiko ya wazazi na wanaharakati waliosema vitambulisho hivyo ni vya kibaguzi, Shule ya Upili ya Northcliff mjini Johannesburg wiki hii imelazimika kuondoa kitambulisho hicho.

Waziri wa Elimu wa Mkoa wa Gauteng, Panyaza Lesufi amesema amezungumza na mkuu wa chuo hicho ambaye ameafiki kubatilisha kadi au kitambulisho hicho maalumu.

Mwanaharakati wa kijamii Yusuf Abramjee amesema aliwasilisha malalamiko kwa waziri huyo kufuatia malalamiko ya wazazi. Naye Abeedah Adams, mzazi katika shule hiyo amesema bintiye alilazimika kubeba kitambulisho hicho kila wakati alipokuwa shuleni ili kuruhusiwa kuvaa hijabu. Amelinganisha kitendo hicho na sera za mfumo wa ubaguzi wa rangi uliokuwepo Afrika Kusini ambapo wazalendo weusi walilazimishwa kubebe vitambulisho maalumu kusafiri kutoka mji moja hadi mwingine. Abramjee amesema wazazi wamempongeza waziri wa elimu kwa kuchukua hatua za haraka kuhusu suala hilo.Shule Afrika Kusini yakosolewa kuanzisha kitambulisho cha wenye kuvaa Hijabu

Katiba ya Afrika Kusini inaruhusu uhuru wa kuabudu na inapinga ubaguzi wowote kwa msingi wa kidini.

Waislamu ni zaidi ya asilimia mbili ya watu wote milioni 50 Afrika Kusini na wanashiriki katika sekta zote za kiuchumi nchini humo.

3607696

captcha