IQNA

Mji wa Kale wa Kiislamu wagunduliwa Ethiopia

14:50 - June 18, 2017
Habari ID: 3471024
TEHRAN (IQNA)-Wataalamu wa akiolojia wamegundua mji wa kale wa Kiislamu ambao ulikuwa kituo cha kibiashara zaidi ya miaka 1,000 iliyopita

Wanaakiolojia wanasema mji huo wa kale, ulio karibu na mji wa pili kwa ukubwa wa Ethiopia wa Dire Dawa, unaweza kuchangia katika kufahamu chimbuko la Uislamu katika nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika. Watafiti wanaamini kuwa mji huo ulio katika eneo la Harlaa mashariki mwa Ethiopia ulijengwa katika karne ya 10 Miliadia (CE) na unajumuisha majengo yaliyojengwa kwa mawe huku baadhi ya wenyeji wa eneo hilo wakisimulia ngano za kale zisemazo mijitu mikubwa ilikuwa ikiishi sehemu hiyo. Kwa mujibu wa wanaakiolojia, mji huo wa kale ulikuwa na utajiri mkubwa na unajumuisha pia msikiti unaoaminika kujengwa karne ya 12 CE pamoja na makaburi.

Aidha kuna vyombo vya kale ambavyo vinaaminika kutoka Madagascar, Maldives, Yemen na China pamoja na sarafu za shaba na fedha zilizotoka Misri na zenye maandishi yanayoashiriki zilitumika karne ya 13 Miladia. Mtafiti Timothy Insoll wa Chuo Kikuu cha Exeter cha Uingereza, aliye katika mradi wa kuchimbua mji huo wa kale, anasema kiwango cha juu cha vito vilivopatikana viliundwa katika eneo hilo kwa kutumia madini yenye thamani kama vile shaba, fedha n.k kwa kutumia teknolojia ya India. Anasema wategeneza vito kutoka India yamkini waliiishi katika mji mkubwa wa Harlaa ambao ulikuwa na wakaazi wa mataifa mbali mbali. Aidha wataalamu wanasema msikiti katika mji huo wa kale unashabihiana na misikiti ya kale iliyoko mwambao wa Afrika Mashariki hasa Tanzania na Somaliland na hilo linaaashiria kuwa wakaazi wa Harlaa walikuwa na mahusiano na jamii zinginezo za Kiislamu barani Afrika.

Uislamu ulifika nchini Ethiopia (Abyssinia au Al Habash) takribani mwaka 613 Miladia (CE) wakati wa uhai wa Mtume Muhammad SAW alipoona mateso ya aliwaambia: "kama mngeondoka kwenda Abyssinia (ni bora zaidi kwenu), kwa sababu mfalme (wa kule) hatavumilia uonevu, na nchi hiyo ni rafiki, hadi hapo Mwenyezi Mungu atakapo waondolea dhiki."

Wataalamu wanasema mji wa kale wa Harlaa ni ushahidi wa kuwepo uhusiano wa Ethiopia na Ghuba ya Uajemi, India na Afrika Kaskazini.

Hivi sasa Waislamu wanakadiriwa kuwa Waislamu wanakadiriwa kuwa takriabani asilimia 40 ya idadi ya watu milioni 99 nchini Ethiopia.

Mji wa Kale wa Kiislamu wagunduliwa Ethiopia


Mji wa Kale wa Kiislamu wagunduliwa Ethiopia

3610437

captcha