IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Siku ya Kimataifa ya Quds in umuhimu mkubwa, ni siku ya kupinga Wazayuni, Mabeberu

10:32 - June 22, 2017
Habari ID: 3471030
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei ameitaja Siku ya Kimataifa ya Quds kuwa yenye umuhimu mkubwa.

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei ameitaja Siku ya Kimataifa ya Quds kuwa yenye umuhimu mkubwa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyasema hayo Jumatano alasiri mjini Tehran alipokutana na wahadhiri, watafiti na wasomi wa vyuo vikuu vya Iran na kuongeza kuwa: "Siku hii mbali na kuwa ni siku ya kuunga mkono taifa lililodhulumiwa pia ni nembo ya kupambana na uistikbari na ubeberu duniani."

Akiashiria Siku ya Kimataifa ya Quds inayoadhimishwa Ijumaa, Kiongozi Muadhamu aliongeza kuwa: "Kuadhimisha Siku ya Quds hakumaanishi tu kutetea taifa lililodhulumiwa na kutimuliwa kutoka nyumba zao, bali leo kutetea Palestina ni kutetea ukweli ambao ni zaidi ya kadhia ya Palestina."

Akibainisha kuhusu umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Quds, Ayatullah Khamenei amesema,"Siku ya Quds ni muhimu sana. Si siku tu ya kutetea tu taifa madulumu ambalo limefurushwa kutoka ardhi zao. Kwa hakika sisi tunapambana na mfumo dhalimu wa kisiasa na wa kiistikbari. Leo kutetea palestina ni kutetea ukweli. Ni ukweli mpana zaidi ya kadhia ya Palestina. Leo kupambana na utawala wa Kizayuni ni kupambana na uistikbari na mfumo wa ubeberu. Leo tunaona kuwa uukizungumza dhidi ya utawala wa Kizayuni, watawala wa Marekani wanahisi wewe ni adui na hasimu. Kwa hivyo Siku ya Quds inapaswa kuadhimishwa na maandamano ya Siku ya Quds ni muhimu sana."

Kwa upande wake, Akizungumza Jumatano katika kikao cha baraza la Mawaziri, Rais Hassan Rouhani alifafanua kuhusu umuhimu wa Siku ya Quds na kusema, "Moja ya Fursa ambazo Mapinduzi ya Kiislamu yametuletea katika Mwezi wa Ramadhani ni kutumia Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama Siku ya Quds na kuhuisha kadhia ya Palestina. Taifa la Iran na mataifa mengine duniani, Waislamu na wengine huheshimu Siku ya Quds ili ulimwengu usisahau kadhia ya Palestina. Maudhui ya Palestina ina umuhimu kwetu Waislamu na walimwengu wote. Katika kipindi cha miaka 70 sasa watu wa Palestina na eneo wamekuwa wakipata masaibu, hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel ambao ni utawala ghasibu, wa kidalimu na utendao jinai. Kwa hakika ni utawala wa ubaguzi wa rangi."

Wiki hii Mamilioni ya watu kote duniani wanatazamiwa kujitokeza kwa wingi kwa munasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo inafanyika Ijumaa kwa lengo la kuwaunga mkono Wapalestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel. Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na hayati Imamu Ruhullah Khomeini kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds na kuwataka Waislamu kote duniani kushiriki katika maandamano ya siku hiyo ili kuonesha hasira zao dhidi ya siasa za kibaguzi za Israel huko Palestina.Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itaadhimishwa Ijumaa Juni 23. Wananchi wa Iran wanatazamiwa kujiunga na watu wa maeneo mengine duniani na kujitokeza kwa mamilioni katika maandamano hayo ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo yatafnayika mjini Tehran na katika miji yote mikubwa na midogo kote Iran.

3612213

captcha