IQNA

Msikiti wa Manchester wahujumiwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu+PICHA

10:56 - July 18, 2017
Habari ID: 3471072
TEHRAN (IQNA)-Watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wameushambulia na kuuharibu vibaya msikiti katika mji wa Manchester, Uingereza.

Taarifa zinasema msikiti huo ambao unafahamika kama Kituo cha Kiislamu cha Nasafat mjini Manchester uliharibiwa vibaya katika moto ulioteketeza baadhi ya sehemu zake Jumapili usiku, huku vyumba vitatu vya masomo vikiharibiwa vibaya.

Polisi mjini Manchester wanasema wanafanya uchunguzi kuhusu jinai hiyo ili kubaini walioitekeleza.

Msikiti huo ulio katika eneo la Newton Heath uliwahi kulengwa katika hujuma ya watu wenye chuki dhidi ya Uislamu. Monsurat Adebanjo-Aremu katibu wa kituo hicho cha Kiislamu amesema wanaopinga Uislamu waliwahi kukojoa katika ukuta wa jengo la msikiti na kurusha vichwa viwili vya nguruwe ndani ya msikiti huo Waislamu wakiwa wanaswali.

Amesema katika hujuma ya Jumapili mbali na vyumba vitatu kuharibiwa vibaya pia kuna uharibifu katika ukumbi mkuu wa msikiti.

Taarifa zinasema wazimamoto walifika katika msikiti huo saa sita kasorobo na kuuzima moto na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Nchini Uingereza katiak miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu baada ya kujiri hujuma za kigaidi ambazo kundi la kigaidi la ISIS limedai kuhusika nazo. Viongozi wa Kiislamu Uingereza wamesisitiza mara kwa mara kuwa Uislamu hauna uhusiano na ugaidi na kwamba wanaotekeleza ugaidi sio Waislamu. Aidha baadhi ya weledi wa mambo wanasema makundi ya kigaidi kama vile ISIS yameanzishwa na mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi na Wazayuni kwa lengo la kuuharibia Uislamu jina duniani.

Msikiti wa Manchester wahujumiwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu+PICHA


Msikiti wa Manchester wahujumiwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu+PICHA


Msikiti wa Manchester wahujumiwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu+PICHA



3463387

captcha